RC KINDAMBA AWAAGIZA MA DC KUTOA ELIMU YA LISHE.
Na. Nicholas Ndabila
SONGWE: Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Waziri Kindamba amewataka wakuu wa Wilaya kwenda kutoa elimu ya lishe kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa ametoa maagizo hayo wakati akiwasainisha mikataba ya lishe wakuu wa Wilaya leo Oktoba 5 wakati wa kikao cha tathimini wa afua mbalimbali za Afya kwa Mkoa wa Songwe.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Waziri Kindamba amesema si jambo zuri kwa Mkoa wenye fursa za Kilimo kutajwa kuwa na idadi kubwa ya udumavu wa watoto.
Mkuu wa Mkoa amewataka wakuu wa Wilaya kufanya mabadiliko kupitia mikata waliosainiwa, mnatakiwa mkapambane kuhakikisha mnatoa elimu na kueleza jamii namna bora ya kutumia lishe iliyo na mchanganyiko wa virutubisho vyote vinavyo hitajika na mwilini.
Mhe. Waziri Kindamba amesema Watu wengi tunakula chakula kwa sababu tumbo linahitaji lakini hatuzingatii mchanganyiko bora wa vyakula vyenye viini lishe na virutubisho vyote, kwa kufanya hivi hatuwezi kuwa na Afya bora kama tutaendelea kula kwa mazoea.
"Unamkuta mtoto mdogo ana kitambi kuliko mtu aliye ajiriwa katika kampuni au taasisi ukimuuliza unafanya kazi katika kampuni gani anashindwa kujibu kwanini kwa sababu hatujazingatia lishe na mpangilio mzuri wa chakula cha kuwapa watoto wetu " Mhe. Waziri Kindamba.
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Bi. Happiness Seneda amesema bado Mkoa haufanyi vizuri kwenye maswala ya lishe, inahitajika jitihada kubwa ili kuliondoa janga la udumavu wa akili kwa watoto pamoja na magonjwa yanayosababishwa na ukosefu wa lishe.
Elimu itolowe kwa wananchi na familia ili kuhakikisha wanapata chakula kilicho na mchanganyiko wa makundi yote matano, amesema, Bi. Happiness Seneda.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wamesema wanapenda kuona Songwe unabaki kuwa Mkoa wa mwisho kwa kuundwa lakini si katika jambo lingine lolote lile la kimaendeleo, wamewaagiza wakuu wa Wilaya kuchukua dhana hiyo kwa kufuatili jambo la lishe kwa ukaribu zaidi ili Mkoa uondokane na adha ya magonjwa ya lishe.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.