RC KINDAMBA NA KAMPENI YA PANDA MTI, ZUIA KUKATA MTI.
SONGWE: Serikali ya Mkoa wa Songwe inampango wa kuanzisha kampeni maalumu ya kupanda miti na kuzuia kukata miti ili kunusuru uharibifu wa mazingira unaoendelea hapa Mkoani.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Waziri Kindamba amesema hayo wakati wa kikao kazi cha viongozi wafanya maamuzi (uragabishi) kilichofanyika Oktoba 17 na kuhudhuriwa wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama Mkoa na watalamu ngazi Mkoa.
Mhe. Waziri Kindamba amesema atakutana wawikilishi wa wananchi ngazi ya Kata waheshimiwa Madiwani wote pamoja na viongozi wa Chama cha Mapinduzi, wadau wengine kuona namna ya kufanikisha kampeni ya upandaji miti na kuzuia kukata miti ili kutunza Mazingira ya Mkoa.
Baada ya kukaa na makundi hayo, nategemea kuona kila kaya inapanda miti, kuona miti inapandwa kwenye maeneo yetu mbalimbali, amesema, Mhe. Waziri Kindamba.
"Ukipita katika milima mingi na misitu yetu ya Songwe utaona jinsi miti ilivyokatwa na kuacha vipara tu, unakutana na mtu amejenga Nyumba nzuri lakini hakuna mti hata mmoja uliopandwa hali hii inaweza kupelekea upungufu wa mvua na mafuriko kwa kukosekana kwa miti" Mhe. Waziri Kindamba.
Pia, Mkuu wa Mkoa, Mhe. Waziri Kindamba amesema kumekuwepo na matukio mengi ya Nyumba za watu kuezuriwa na upepo au mafuriko kwa baadhi ya maeneo katika kipindi hiki ambacho tunaenda kwenye msimu wa Mvua kutokana na ukosefu wa miti katika kaya na sehemu za misitu yetu kwa sababu ya uharibifu wa mazingira unaoendelea kwa sasa.
Sisi viongozi pamoja na watalamu kwa maeneo tunayoishi lazima tutoe elimu kwa wananchi wetu juu ya umuhimu wa kutunza mazingira, amesema Mhe. Kindamba.
Wakati huohuo, Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wananchi kujenga vyoo bora na kuvitumia kwa usahihi ili kujiepushe na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu ambacho kinaweza kutokea.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.