• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
SONGWE REGION
SONGWE REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa MKOA WA SONGWE

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Sehemu
      • Mipango na Uratibu
      • Idara ya Elimu
      • Huduma za Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
  • Wilaya
    • Mbozi DC
    • Songwe DC
    • Momba DC
    • Ileje DC
  • Halmashauri
    • Mbozi
    • Ileje
    • Momba
    • Songwe
    • Tunduma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Mifugo
    • Madini
    • Kilimo
    • Biashara
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya na Ustawi Wa Jamii
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma ya Mifugo na Uvuvi
    • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
    • Mipango na Takwimu
    • Ujenzi
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Utaratibu
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC MAKAME APONGEZA UTENDAJI WA MAHAKAMA YA TANZANIA ASEMA NI NGUZO YA MAENDELEO

Posted on: February 2nd, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Jabiri Makame leo tarehe 02 Februari 2026 ameongoza Maadhimisho ya Siku ya Sheria mkoani Songwe, ambapo ametumia fursa hiyo kuipongeza Mahakama Kuu ya Tanzania chini ya Jaji Mkuu Mhe. George Masaju pamoja na mahakimu wote wa Mkoa wa Songwe kwa kuungana na Mahakama Kuu ya Tanzania kuadhimisha Siku ya Mahakama Duniani, chini ya kauli mbiu “Mchango wa Mahakama katika Ustawi na Maendeleo ya Taifa.”


Akizungumza katika maadhimisho hayo, RC Makame amesema ili kuwepo ustawi na utawala bora ni lazima kuwe na mgawanyo wa majukumu na madaraka, akisisitiza kuwa Tanzania inajivunia muhimili wa kimahakama kwa kuendelea kutekeleza majukumu yake ipasavyo.


Ameeleza kuwa muhimili huu ni nguzo muhimu katika kuvutia uwekezaji kwani hujenga imani na uhakika wa usalama wa mitaji, sambamba na kuwa msingi wa kutatua changamoto za kisiasa kwa haki na usawa.


Aidha, amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa, TAKUKURU, madalali wa mahakama pamoja na wadau wote kushirikiana kwa karibu na muhimili wa mahakama ili kuongeza ufanisi na kupunguza malalamiko mbalimbali yanayojitokeza katika utoaji wa haki. Amesema kila mdau ana wajibu wa kusaidia kuimarisha mifumo ya haki kwa maslahi mapana ya wananchi.


Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS – Songwe Chapter), watumishi wa mahakama, viongozi wa dini, machifu pamoja na wadau mbalimbali, RC Makame amesema Serikali ya Mkoa haita kuwa kikwazo katika kusaidia shughuli za kimahakama, bali itaendelea kushirikiana na kuongeza michango ili kuinua na kuboresha utoaji wa huduma za haki mkoani Songwe.


Kwa upande wake, Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Chami, amesema maendeleo ya teknolojia yamekuwa nguzo muhimu katika kurahisisha shughuli za kimahakama, akibainisha kuwa matumizi ya mifumo ya TEHAMA yameongeza ufanisi, uwazi na upatikanaji wa haki kwa wananchi.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI January 30, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RC MAKAME APONGEZA UTENDAJI WA MAHAKAMA YA TANZANIA ASEMA NI NGUZO YA MAENDELEO

    February 02, 2026
  • RC MAKAME AONGOZA JUKWA LA WADAU WA KILIMO MKOANI SONGWE.

    November 19, 2025
  • RC CHONGOLO AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI WILAYA YA MOMBA KUJADILI HOJA ZA CAG

    June 11, 2025
  • RC CHONGOLO AONGOZA KIKAO CHA KUJADILI HOJA ZILIZO BAINISHWA KATIKA RIPOTI YA CAG HALMASHAURI YA MBOZI

    June 10, 2025
  • Angalia zote

Video

ELIMU KWA WATOTO KIPINDI CHA CORONA
Video za Ziada

Kurasa za Karibu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • SALARY SLIP PORTAL
  • AJIRA

Kurasa Mashuhuri

  • IKULU
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE

    Simu: 025 2580305

    Simu ya Kiganjani: 025 2580305

    Barua pepe: ras@songwe.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.