RC MGUMBA AMUONYA AFISA ELIMU SEKONDARI KWA KUMDANGANYA.MBOZI:
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amemuonya Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kwa kumudanganya juu ya ujenzi wa Sekondari ya Ichenjezya.Afisa Elimu Sekondari alimudanganya Mkuu wa Mkoa wakati akiwa kwenye ziara ya ukaguzi wa miradi katika Sekondari ya Senye iliyopo Kata ya Vwawa baada ya Mkuu wa Mkoa kuhoji sababu iliyosababisha Halmashauri kujenga Sekondari Kata ya Vwawa na kuacha kujenga Kata ya Ichenjezya ambayo haina Sekondari na muongozo wa unataka kipaombele cha kwanza Shule ikajengwe kwenye Kata ambayo haina Sekondari.Mkuu wa Mkoa alipomuuliza kwa nini hawajajenga Kata ya Ichenjezya, Afisa Elimu akasema hawajajenga kwa sababu Ichenjezya wana eneo dogo la ekari 4, eneo ni oevu, maji yanajaa katika eneo ilo, watalamu walisema eneo halifai, eneo liko Kata ya Hasanga na sio Ichenjezya mwisho wasingeweza kupeleka fedha za Serikali kwenye ujenzi Sekondari kwa sababu izo.Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba kukatisha ziara yake na kuamua kwenda Kata ya Ichenjezya na kujionea hali halisi akakuta taarifa aliyopewa na Afisa Elimu Sekondari ni tofauti na uhalisia uliopo.Mkuu wa Mkoa amekuta eneo la Shule ya Sekondari lina ekari 8, maboma ya shule yamejengwa tangu 2019 na Halmashauri imepeleka fedha takribani Milioni 10 pamoja na wadau wengine wamechangia.Kufuatia hali iyo, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba ameuagiza Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kuhakikisha wanafanya jitihada za kukamilisha Sekondari ya Ichenjezya ili ianze kufanya kazi.Tusiwaachie wananchi peke yako katika ujenzi huu Halmashauri ongezeni nguvu ili mradi huu uishe haraka.Diwani viti maalumu Tarafa ya Vwawa, Mhe. Neema Nzowa amemshukuru Mkuu wa Mkoa Kwa ziara yake na amemuomba asaidie kufanikisha ukamilishaji wa Shule.Diwani wa Kata ya Ichenjezya, Mhe. Bahati Mbughi amesema walipolibaini eneo waliwaita watalamu na wakasema linafaa kujenga Shule na tukaletewa ramani ya Shule na Halmashauri ilimtuma injinia kuja kusimamia ujenzi wa msingi.Wananchi wamechangia nguvu kazi za thamani ya shilingi Milioni 13 na wametoa ushirikiano wa kutosha katika ujenzi na wao ndio wamekuwa wakichota maji na shughuli nyingine za ujenzi kama kuchanganya zege.Mtendaji wa Kata ya Ichenjezya, Bi. Atupakisye Malakalinga amesema hadi sasa nguvu za wananchi ni Milioni 13.6, Halmashauri imeleta Milioni 10 pamoja na bati 270, mfuko wa jimbo bati 54 na saruji 104, Mbunge wa Jimbo la Vwawa mifuko 25 ya saruji na Kamati ya elimu 210,000.Malengo yetu ni ifikapo januari 2023 Shule ianze kufanya kazi kutokana na wananchi wanamuitikio mzuri.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.