RC MGUMBA ASHIRIKI IBADA YA KUMUWEKA WAKFU ASKOFU MWAKIHABA.TUKUYU: Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba ameshiriki ibada ya kumuweka wakfu na kumsimika Askofu wa awamu ya tano Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Konde, Askofu Geoffrey Samwel Mwakihaba pamoja na msaidizi wake Mch. Dkt. Meshack Edward Njinga katika ibada iliyofanyika Usharika wa Tukuyu, 5 Juni 2022.Ibada imeongozwa na Kiongozi Mkuu wa Kanisa la KKKT Tanzania, Askofu Dkt. Fredrick Shoo na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Juma Homera aliyemuwakilisha Mhe. Samia Suluh Hasani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.