Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amewataka watalamu wa lishe na Afya waliopo katika vijiji, Kata, Wilayani na Mkoa kutoa elimu ya kula chakula bora kwa wananchi ili kuondokana na hali ya udumavu iliyopo Songwe.
"Elimu ijikite kwa madhara ya kutokula chakula bora ili wananchi wabadili utamaduni wa kula chakula ambacho sio bora" Omary Mgumba.
Mhe. Mgumba amesema wananchi wapewe elimu ata kama hapendi chakula icho kutokana na tamaduni zetu tuwaeleze umhimu wa kula chakula icho, taratibu watabadilika kwani Songwe hakuna shida ya chakula.
Mkoa wa Songwe unashika nafasi ya 3 katika uzalishaji wa chakula hapa Tanzania lakini hali ya udumavu kwa watoto chini ya miaka 5 ni 43.3% hali inayosababishwa na wananchi kukosa elimu ya chakula bora.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.