RC MGUMBA ATOA SIKU 7 HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO ZIANZE KUTOLEWA HOSPITALI YA RUFA
SONGWE: Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba ametoa siku saba kwa uongozi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Songwe kuanza kutoa huduma ya mama na mtoto katika hospitali mpya ya rufaa iliyopo Hasamba.
Mkuu wa Mkoa ametoa agizo hilo alipofanya ziara ya ukaguzi wa shughuli za ujenzi pamoja na huduma katika Hospitali mpya ya rufaa ya Mkoa, 2 Juni 2022.
Mkuu wa Mkoa amesema anataka kuona huduma ya Mama na mtoto zinaanza haraka ndani ya siku saba na watalamu wote wa afya wa ngazi ya Mkoa wahamia mara moja katika Hospitali mpya ya rufaa ya Mkoa ili Serikali ijue mapungufu yaliyopo katika Hospitali ya Vwawa na kutatua haraka kabla ya kufika Julai 2022.
“Halmashauri ya Mbozi imetufadhili Mkoa vya kutosha ni muda sasa Mkoa kuhamia katiak Hospitali hii na serikali ione upungufu uliopo katika Hospitali ya Vwawa na kushugulikia mapungufu ” Mhe. Omary Mgumba.
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Mkoa, Dkt Ahmed Ramadhan amesema hadi sasa wagonjwa 1,163 wamepata huduma kwa upande wa wagonjwa wa nje tu na wagonjwa 12 wamepata huduma ya kulazwa.
Ingawa wodi hazijakamilika ziko kwenye ujenzi, lakini uongozi wa Hospitali tuliamua kutenga baadhi ya vyumba kwenye jingo la wagonjwa wa nje na kuvigeuza wodi kwa wale wagonjwa ambao watahitajika kulazwa, amesema Dkt. Ahmed.
Aidha, Dkt. Ahmed amesema ifikapo Julai 2022 baada kukamilisha jengo la wagonjwa wa dharura na maututi huduma kwa watoto njiti ambao wamezaliwa kabla ya miezi tisa kufika pamoja na kutoa huduma kwa wagonjwa wa dharura zitaanza kutolewa.
“Watoto wanaozaliwa kabla ya miezi tisa tumekuwa tunawapeleka Mkoa wa Mbeya pamoja na wale wagonjwa maututi nah ii ni kutokana Mkoa wa Songwe tulikuwa hatuna miundombinu ya kuwahudumia lakini kwa sasa majengo haya ya wagonjwa maututi na dharura kukamilika wagonjwa watapata huduma hapa hapa” Dkt. Ahmed.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amesema ndani ya mwaka mmoja Rais Samia Suluh Hassan ameleta fedha zaidi ya shilingi Bilioni 8.5 katika Hospitali ya Mkoa tu kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo la wagonjwa wa nje, ujenzi wa jengo la mama na mtoto, jengo la dharura na maututi pamoja na nyumba ya mtumishi.
Mkuu wa Mkoa ameuagiza uongozi wa Hospitali kukamilisha majengo ya dharura, maututi na nyumba ya mtumishi kabala ya kufika Julai 2022 na jengo la wodi za mama na mtoto lilamilike kabla ya kufika oktoba 2022 na kumtaka mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa ameuagiza uongozi wa Hospitali wakati majengo yanakamilishwa na vifaa tiba vyote ambavyo vimeagizwa navyo viwe vimefika kabla ya kufika Julai 2022 na huduma zianze haraka.
MWISHO
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.