RC MGUMBA AVUNJA KAMATI ZA UJENZI KITUO CHA AFYA MPANDE WATALAMU WASIMAMISHWATUNDUMA:
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amezivunjwa kamati zote za ujenzi wa kituo cha Afya mpande pamoja na watalamu wanaosimamia ujenzi huo, kamati zilizovunjwa ni Kamati ya ujenzi, mapokezi na manunuzi.Mkuu wa Mkoa amechukua hatua hiyo leo Juni 8 wakati wa ziara ya ukaguzi wa mradi katika kituo cha Afya Mpande ambacho Serikali imeleta fedha shilingi milioni 300 na ujenzi ukiwa ndio uko hatua ya awali na kukuta bei za vifaa walizoweka ni kubwa kuliko bei ya soko.Diwani wa Kata ya Mpande, Mhe. Salum Kiambi amesema walikubaliana na wana kamati kwamba vitu ambavyo vitaletwa kwa bei ya juu visichukuliwe na ndio maana walipooana ndoo ndogo inanuliwa kwa bei ya 13,000 badala ya 5,5000, mipira ya 250,00 wameandika 280,000, sururu ya 8,000 wamenunua kwa 13,000 zinanuliwa kwa bei ya juu na nilipoenda ofisi ya manunuzi waliniambia wameisha andaa kotesheni tayari.Mtendaji wa Kata namsimamisha kwa sababu amenisomeaa taarifa ya uongo ambayo haina ukweli, hivyo mtendaji wa Kata pamoja na watalamu walioshirikiana kuandaa taarifa na kuratibu ujenzi wa kituo cha Afya Mpande wote wakae pembeni kupisha uchunguzi tukiwaacha hawa Kituo cha Afya hakitaisha kabisa amesema Mhe. Omary Mgumba.Mtendaji wa Kata, Enock Mabina anasema yeye aliandaa taarifa yake lakini Ofisi ya mipango wakamletea taarifa ambayo wameandaa ili aweze kuisoma na kudai taarifa yak wake ina utofauti na iliyotoka ofisi ya mipango.Mkuu wa Mkoa ametoa siku 7 kwa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mji Tunduma kuunda kamati ambazo zinatokana na wananchi halisi na sio kamati za ujanja ujanja, kamati zijimuishe wananchi wa Kata zote.Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa watendaji wote ndani ya Mkoa wanapopata maelekezo aa maagizo kutoka kwa viongozi wao ni vyema wapate maagizo yakiwa katika maandishi ili badae wasijekurukwa na wakabaki wao tu.MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.