RC MGUMBA AWATOA HOFU WAMACHINGA UJENZI WA SOKO TUNDUMA.SONGWE: Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amewatoa hofu wamachinga ambao watakosa eneo katika ujenzi wa soko linaloendelea la majengo katika mji wa Tunduma.Mkuu wa Mkoa amesema Serikali itaendelea kujenga masoko lengo ni kuhakikisha kila mfanyabiashara mdogo anapata sehemu nzuri ya kufanyika kazi katika masoko rasmi na kutatua changamoto za wamachinga.Mkuu wa Mkoa amesema hayo alipokutana na viongozi wa shirikisho la wamachinga Mkoa wa Songwe ofisini leo Mei 26."soko la majengo ni mwanzo tu, likimalizika Serikali itajenga na lingine hatutaki kujenga masoko mengi kwa wakati moja alafu tushindwe kumaliza na kubaki magofu tunataka tukianza kujenga na tunamaliza moja kwa moja" amesema Mhe. Omary Mgumba.Aidha, Mkuu wa Mkoa amesema wakati ujenzi wa soko la mejengo unaendelea, pia tunaendelea kukamilisha stendi ya Mpemba ambayo tayari kuna eneo maalumu kwa wamachinga, eneo maalumu kwa minada hivyo kila machinga atapata fursa ya kufanya biashara.Pia kuhusu madereva wa malori Mkuu wa Mkoa amesema nao wanatengewa sehemu maalumu karibu na sehemu wanakopaki magari yao kwa ajili ya kununua bidhaa mbalimbali ili watakapokuwa wamepaki wanajua sehemu fulani anakwemda kununua bidhaa na sio barabarani tu.Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wamachinga kutofanya biashara barabarani kutokana na hatarii zilizopo za ajali, matukio ya moto pamoja na kutofanya biashara mbele ya Nyumba ya mtu.Kwa upande wao viongozi wa shirikisho la wamachinga Mkoa wa Songwe wameishukuru Serikali ya Rais Samia Suluh Hassan kwa kuwajali kwa vitendo kwa kutoa fedha Milioni 10 kwa kila Mkoa kwa ajili ya kuimarisha shirikisho la wamachinga na wamachinga.Katibu wa Shirikisho la wamachinga Mkoa wa Songwe, Judith Msemwa amesema lengo la shirikisho ni kutoa elimu kwa wamachinga wanaotembea ili angalau awe Kuna sehemu ambayo Serikali inamtambua na aweze kunufaika na fursa zinazotoka Serikali kama mkopo.Mwenyekiti wa Shirikisho la wamachinga Mkoa wa Songwe, Kelvin Kyando amesema tunataka wamachinga wawe wazalendo kwa nchi yao ikiwa ni pamoja na kujitokeza kwenye baadhi ya shughuli za umma na kuchangia baadhi ya ushuru kwa Halmashauri ambao ni rafiki kwa wamachinga.Elizabeth Mwasandube ambaye ni mfanyabiashara maarufu kama machinga amesema kwa sasa Serikali inafanya kazi kwa karibu na ushirikiano na viongozi wa machinga na hakuna manyanyaso.MWISHO
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.