RC MGUMBA AZIJULIA HALI FAMILIA ZIZOPOTEZA NDUGU KWA MAPOROMOKO YA UDONGO.ILEJE: Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amefika Kata ya Sange na Ngulugulu kutoa pole kwa familia mbili (2) ambazo zimepoteza ndugu zao watano (5) kutokana na maporomoko ya udongo kuangukia Nyumba zao baada ya mvua kubwa kunyesha mfulilizo.Mnamo usiku wa kuamkia 29 Aprili 2022 wananchi wapatao watano (5) kutoka Kata ya Sange na Ngulugulu walipoteza maisha wakiwa wamelala kwenye Nyumba zao na kuangukiwa na maporomoko ya udongo."Kwa niaba ya Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluh Hassan na Serikali yake tunatoa pole kwa familia zote na jambo la muhimu tunaendelea kumuomba Mungu awape subra na uvumilivu katika wakati mgumu huu muliokuwa nao" Mhe. Omary Mgumba.Aidha, Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wananchi wa Ileje ambao wanaishi sehemu za muiniko kuchukua tahadhari katika kipindi ambacho mvua zinazoendelea kunyesha.Thobias Amenye Shibanda baba aliyepoteza watoto 2 na mjukuu mmoja amemshukuru Mkuu wa Mkoa na timu yake kwa kuja kumfraji baada ya msiba mzito uliomtokea.Zawadi Kabuje mwananchi wa kijiji cha Sange ameishukuru Serikali kwa kuwa karibu na familia zilizopata maafa.Waliofariki kutoka Kata ya Ngulugulu ni Eliudi Kajange (26) na mdogo wake Faraja Kajange(18) wa Kijiji Cha Kisuga na kutoka Kata ya Sange ni waliofariki ni mjamzito Rozalia Kijalo (22) Lazaro Shibanda (22) na mtoto anayeitwa Ayubu Shibanda (4).Wenyeji wa eneo ilo wanadai maporomoko ya udongo ya aina hii yaliwai kutokea mwaka 1984 eneo la lusalala na Ngulugulu na kusabisha vifo vya watu 3.Serikali inaendelea na zoezi la kufungua Barabara ambazo zimezibwa na maporomoko ya udongo ili ziweze kupitika kama awali.MWISHO
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.