Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amezitaka Halmashauri za Songwe kutumia mapato ya ndani kutatua shida za wananchi katika kuwasogezea jirani huduma za jamii kwa kutekeleza miradi.
Wito huo umetolewa 29 Mei wakati Mkuu wa Mkoa akiongea na watumishi wa Wilaya ya Mbozi."Halmashauri zijenge Zahanati, Shule, vituo vya Afya kwa kutumia mapato yake sio kusubiria fedha kutoka Serikali Kuu tu ndio zije kujenga vitu vipya" Omary Mgumba.
Mhe. Mgumba amesema Halmashauri ikiwa inajenga kituo cha Afya kwenye na Serikali kuu itajenga kwenye Kata nyingine, hivyo itasaidia kutatua au kupunguza changamoto kwa wananchi.
Pia, Mkuu wa Mkoa amezitaka Halmashauri kutumia fedha kwa kufuata mipango iliyopo kwenye Bajeti.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.