RC MICHAEL AMTAKA DED ILEJE KUCHUKUA HATUA KALI KWA WANAOKWAMISHA MIRADI.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Dkt. Fransis Michael amemtaka Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Ileje kuwachukulia hatua watumishi watakaobainika wanamkwamisha katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mkuu wa Mkoa ametoa maagizo hayo kwa Mkurugenzi wa Ileje, Bi. Nuru Kindamba wakati wa Baraza la kujadili Hoja za Mdhibiti na na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) lililofanyika Juni 15 wilayani Ileje.
Mhe. Dkt. Francis Michael amemwambia Mkurugenzi wa Ileje kuwa mtumishi atakayemkwaza au kumyumbisha asifike malengo awasilishe majina ofisini kwake kwa hatua zaidi za kisheria.
"Tukibaini mtumishi anafanya kwa uzembe tutamchukulia hatua na kama liko ndani ya uwezo wa mtumishi basi tutamuwezesha" Mhe. Dkt. Francis Michael.
Mkuu wa Mkoa, Mhe. Dkt. Francis Michael amesema Halmashauri ya Ileje ina shida kwenye ukamilishaji wa miradi ya maendeleo licha ya juhudi kubwa anazofanya Mkuu wa Wilaya, hivyo amemtaka Mkurugenzi wa Ileje kusimamia kwa nguvu zote miradi ya maendeleo.
Pia, Mkuu wa Mkoa amelitaka Baraza la Madiwani la Ileje kuchukua hatua kwa watumishi wazembe bila kuwaonea.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Songwe, Ndg. Radwell Mwmpashi amesema baadhi ya watumishi hawawajibiki kutekeleza majukumu yao na kuitaka Serikali kuchukua hatua dhidi yao.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Ileje, Mhe. Ubatizo Songa amesema Baraza lake liko tayari kuyasimamia maelekezo yoye pamoja na kuwawajibisha watumishi wazembe ili miradi iende kwa kasi kama lengo la serikali linavyohitaji kupunguza adha Kwa wananchi.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.