RC MWANGELA: ATOA SIKU 7 KWA TAASISI KUWASILISHA MPANGO KAZI WA UTEKELEZAJI WA ILANI
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Brg. Jen. Nicodemus Mwangela ametoa siku saba kwa Taasisi zilizopo Songwe na wakuu wa Idara kuja na mpango kazi wa namna ya kuanza kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2020-2025 pamoja na Hotuba ya Rais aliyotoa wakati wa kufungua Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Viongozi wa Taasisi waliokutana hii leo na Mkuu wa Mkoa baadhi yao ni TANESCO, RUWASA,TARURA, TANROAD, TRA, CAG, TBA, NFRA, PSPF, TEMESA, NMB, TACRI pamoja na Makatibu Tawala wasaidizi kutoka Songwe
Mkuu wa Mkoa ameagiza kila ofisi ya Umma kuwa na Ilani ya CCM 2020-2025 na Hotuba ya Rais aliyotoa wakati wa kufungua Bunge la 12 pia amewakabidhi wakuu wa Taasisi za Songwe Ilani ya CCM na Hotuba ya Rais aliyotoa wakati wa kufungua Bunge la 12 ili waanze utekelezaji katika Taasisi zao.
“Nahitaji Mpango kazi wa kila Taasisi unaokwenda sambamba na Ilani ya CCM 2020-2025 na Hotuba ya Rais katika kutatua kero za Wananchi wa Songwe” Mhe. Brg. Jen. Nicodemus Mwangela
Aidha Mkuu wa Mkoa amesema ahadi zilizotolewa na Serikali kwa wananchi, Taasisi hizo ndio zinatakiwa kuzitekeleza ikiwa ni pamoja na usimamizi wa miradi ya maendeleo iliyo kwenye utekelezaji na ile itakayoanza.
Na kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Dr. Self Shekalaghe akiongea kwa niaba ya wakuu wa Taasisi amesema kila Taasisi itapewa kero za wananchi zilizopo na zitakazo ibuka ili zitatuliwe, na kero hizo zitawasilishwa kwenye kila kikao cha kila robo ya mwaka na kuziwasilisha kwa Mkuu wa Mkoa.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa ameagiza kamati ya usalama Mkoa kuzifuatilia kwa karibu ofisi za TANESCO na RUWASA Mkoa wa Songwe kutokana na kero ya kukatika kwa Umeme mara kwa mara bila sababu za msingi pamoja na kero ya maji kwenye miradi iliyokamilika.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.