Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus E. Mwangela ametoa siku 30 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe kukarabati vyumba viwili vya madarasa katika shule ya Msingi Kininga ambayo ilifungwa kutokana na ubovu wa miundombinu na hivyo kupelekea wanafunzi zaidi ya 200 kukosa masomo.
Brig. Jen. Mwangela ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea shule hiyo na kushuhudia ubovu wa majengo ya madarasa ambapo wakaguzi waliifunga baada ya kuona kuwa ingehatarisha maisha ya wanafunzi.
“Natoa mwezi mmoja kwa halmashauri ya Songwe kujenga vyumba viwili vya madarasa na nitahakikisha ofisi yangu inasimamia na kuchangia ukarabati wa chumba kimoja cha darasa ili wanafunzi wa kijiji hiki cha Mteka wasikose haki yao ya kupata elimu”, amesisitiza.
Ameongeza kuwa baadhi ya madarasa yaliyojengwa awali kwa nguvu za wananchi hayakusimamiwa na wataalamu wa halmashauri na hivyo kupeleka kujengwa chini ya viwango na hivyo basi wana jukumu la kusimamia ujenzi aliouagiza uwe wa viwango.
Kwa upande wao wananchi wa kijiji cha Mteka wamesema tatizo la ubovu wa vyumba vya madarasa haliwahusu wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi Kininga na hivyo ni jukumu la serikali ya kijiji na wadau wengine wa elimu kulitafutia ufumbuzi mapema ili wanafunzi hao wapate haki yao.
Wamesema michakato ya ujenzi wa majengo ya umma ifanyike kwa utaratibu mzuri ili wakandarasi wenye sifa wapatikane na hivyo kujengwa kwa ubora.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.