Vitendo vya rushwa na upendeleo vimepigwa marufuku katika ligi ya mpira wa miguu inayo endelea ambapo jumla ya timu ishirini za Mkoa wa Songwe zinashiriki kutafuta mshindi atakayewakilisha mkoa katika ligi ya mabingwa wa mikoa.
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Michezo Mkoa amepiga marufuku hiyo jana jioni wakati akizindua rasmi ligi hiyo katika uwanja wa Michezo wa CCM Vwawa.
“Sitapenda kusikia Vitendo vya rushwa vimefanyika katika ligi hii ili kuipendelea timu fulani, tunataka kuona timu itakayowakilisha mkoa ikishinda kwa haki, ma refa mjiepushe na kupokea rushwa na kupendelea timu fulani, ushabiki hautakiwi ligi iendeshwe kwa mujibu wa taratibu na kanuni”, amesisitiza Kafulila.
Ameongeza kwa kuwataka wachezaji wote kujituma, kufanya mazoezi, kujiepusha na vitendo vya ngono pamoja na kuzingatia nidhamu kwa viongozi na waamuzi wa katika ligi hilo.
Aidha Kafulila amesema yeye anapenda maendeleo ya michezo hususani mpira wa miguu hivyo ameanzisha mfuko wa kuendeleza michezo wa mkoa ambao uta zisaidia timu mbalimbali pindi zinapokuwa na uhitaji.
Pia ameahidi zawadi kiasi cha shilingi milioni tatu na nusu kwa washindi watatu wa kwanza katika ligi hiyo ambapo mshindi wa kwanza atapatiwa shilingi milioni mbili, mshindi wa pili milioni moja na mshindi wa tatu atapatiwa shilingi laki tano.
Uzinduzi wa ligi ya Mkoa umefanyika kwa mchezo wa mechi kati ya timu ya Vwawa small boys ya Mbozi na Mpira pesa sports club ya Tunduma ambapo timu ya Mpira pesa iliibuka na ushindi wa goli moja bila.
MAELEZO Y
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.