Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Daniel Chongolo , Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso wameshuhudia utiwaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Tunduma,- Vwawa, Kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Eng. Mwajuma Waziri, kwa niaba ya Serikali na Meneja Mradi wa Kampuni ya Ukandarasi ya China (China Civil Engineering Construction Corporation-CCECC), Bw. Ning Yunfeng,
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
|
|
|
|
Tukio hilo limefanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma leo tarehe 20 Machi 2025 ambapo mradi huo kutoka Chanzo cha Maji ya Mto Momba, uliopo Wilaya ya Momba, mkoani Songwe utakaogharimu shilingi bilioni 119.9 za Tanzania.
Akizungumza Mhe. Chongolo amesema Mradi huo utahusisha ujenzi wa chanzo cha maji (Intake) chenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 21.5, ujenzi wa Kituo cha kuchakata na kutibu maji chenye uwezo wa kuzalisha lita 20m kwa siku, ujenzi wa mtandao wa mabomba ya kusafirisha maji yenye kipenyo cha 100mm yenye urefu wa kilometa 96, ujenzi wa matenki ya maji yenye uwezo wa kuhifadhi ujazo wa lita 5m litakalojengwa katika Mtaa wa Uwanjani/Uhuru, Hakmashauri ya Mji-Tunduma, tenki la lita 3m litakalojengwa katika Kijiji cha Ikana na tenki lenye ujazo wa lita 2m litakalojengwa katika Kijiji cha Nkangamo, Ununuzi wa pampu, Ujenzi wa Ofisi na Vitendeakazi vingine.
Akihutubia mamia ya wakazi wa Mkoa wa Songwe waliojitikeza kushuhudia tukio hilo katika Viwanja vya Uwanjani, mjini Tunduma, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, aliwahakikishia wananchi hao kuwa Serikali itatoa fedha zote za kutekeleza mradi huo ambao ni ahadi ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kumtua mama ndoo kichwani.
Kwa upande wake, Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso, alimpongeza Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa kiasi hicho cha fedha takriben sh. bilioni 120, ambazo ni fedha za ndani, kwa ajili ya kuwaondolea adha ya maji wananchi wa Tunduma, Vwawa na Mlowo, watakaofikiwa na mradi huo.
Mradi huo unatarajia kuwanufaisha wakazi 219,309 katika miji hiyo ya Tunduma, Vwawa na Mlowo, ambapo ujenzi wake utachukua miezi 18 kukamilika na kuanza kutoa maji safi na salama.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.