SERIKALI YABORESHA MAKAZI YA ASKARI MAGEREZA, RC MGUMBA AZINDUA NYUMBA MOJA NA KUWAPA PONGEZI KWA USIMAMIZI.
SONGWE: Serikali imetoa Milioni 114 kujenga Nyumba 3 za Askari wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Songwe, ikiwa Milioni 38 imejenga Nyumba ya Mkuu wa Magerea Mkoa na Milioni 76 zimejenga Nyumba moja ya familia 2 kwa ajili ya Askari Magereza.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba amezindua Nyumba moja ya Mkuu wa Magerea Mkoa iliyojengwa kwa miezi 3 hadi kukamilika na Jeshi la Magereza Songwe.
Mkuu wa Mkoa amelipongeza Jeshi la Magereza kwa kufanikiwa kutatua changamoto zinazowakabili wao wenyewe kwenye Makazi.
"Kitendo cha Jeshi la Magereza kuamua kujenga wenyewe Nyumba kimeweza kuokoa fedha zaidi ya Milioni 9.7 ni jambo la kizalemdo na kupongezwa" Omary Mgumba.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Songwe, Robert Jaka amesema kwa sasa Mkoa umejipanga kuanza kujenga Nyumba nyingine 2 kama iliyozinduliwa leo pamoja na kuanza kujenga laini ya Nyumba za Askari kwa kutumia force akaunti na nguvu za Jeshi la Magereza na muda wowote kuanzia sasa zoezi la kufyatua tofali kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Nyumba izo litaanza rasmi.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.