SERIKALI YAFURAISHWA NA MAENDELEO YA KAMPUNI YA GDM KUJIENDESHA KITAASISI
SONGWE: Serikali ya Mkoa wa Songwe imefuraishwa na maendeleo ya kampuni ya GDM yanavyokwenda vizuri tangu walipompoteza mkurugenzi wao marehemu Grivas Mwangoka Julai 2021.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amesema hayo alipofanya ziara Julai 14 ya kuangalia maendeleo ya kampuni ya GDM kwenye kiwanda cha kukoboa kahawa cha Mlowo pamoja na CPU ya kampuni iliyopo ndolezi.
“Kwa niaba ya Serikali nimeridhishwa na maendeleo ya kampuni ya GDM ya sasa nimepita nimekagua kuanzia kwenye CPU hadi hapa kiwandani kwa kweli kampuni iko vizuri nimekuta kahawa ipo kiwandani na ipo kwenye CPU hongereni sana GDM” Mhe. Omary Mgumba.
Nimefanya ziara hapa GDM kwa lengo maalumu kama Serikali kujua Je GDM iko kama zamani vile alivyokuwepo marehemu Grivas Mwangoka au, kwani Serikali tulipata wasiwasi pale gwiji lilipoondoka ghafla tukawa tunajiuliza je kampuni itakwenda kweli kutokana na uzoefu wa makampuni mengi ya wazao mara nyingi hayaendelei pale mwenyewe anapokuwa amefariki amesema Mhe. Omary Mgumba.
Mkuu wa Mkoa amesema hii inaonyesha marehemu Grivas Mwangoka alishirikisha watu wake wa karibu na hii inatakiwa kuwa fundisho au elimu kwa wafanyabiashara na wawekezaji wazao wa kitanzania ni vizuri kujenga taasisi na sio kujijenga wewe mwenyewe, inatakiwa biashara zetu ziende kitaasisi tunawashukuru GDM kwa kujenga kampuni yenu kitaasisi na sasa inaenda mbele zaidi kuliko jana.
Kwa sasa Mkurugenzi wa Kampuni ya GDM ni Richard Grivas Mwangoka na kampuni imeajiri wafanyakazi zaidi ya 600 ambao wanafanya kazi za muda na za kudumu kwenye mashamba ya GDM pamoja na kiwandani.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.