Serikali imekanusha madai ya kuwa wafanyabiashara waMkoa wa Songwe wamehamia Nchini jirani ya Zambia kutokana na utitiri wa kodizisizo rafiki ikiwa ni baada ya uchunguzi wa kina kufanyika kwa muda wa wikimbili.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa amesema, “nilitoamuda wa siku 14 kwa Mkuu wa Wilaya ya Momba ashirikiane na Mamlaka ya mapatoTanzania (TRA) kufanya uchunguzi wa madai hayo kwa kina na taarifa za awali zamatokeo ya uchunguzi huo zinaeleza kuwa hakuna wafanyabiashara waliohamiaZambia kwa kigezo cha utitiri wa kodi”.
Gallawa amefafanua hayo katika mkutano wa Chemba yabiashara, kilimo na uwekezaji (TCCIA) na kuongeza kuwa taarifa kamili yauchunguzi huo itatolewa hapo baadaye.
Ameongeza kuwa kumekuwa na ongezeko la mapato yamakusanyo ya ndani ya halmasahuri, makusanyo ya TRA na mapato ya forodha hivyotaarifa za wimbi kubwa la wafanyabiashara kuhamia nchini Zambia zinakinzana nauhalisia huo.
Wakati huohuo Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawaametumia fursa hiyo kuwataka wafanyabiashara kuwekeza kwenye eneo lakimondo cha Mbozi linalofanyiwa maboresho hivi sasa kwa ajili yamaadhimisho ya siku ya kimondo duniani yatakayofanyika Juni 30, mwaka huu.
Ameongeza kuwa maadhimisho hayo yanahitaja uwekezajiwa miradi mikubwa ikiwemo nyumba za kulala wageni, viwanja vya kisasa vyamichezo, kumbi za starehe, pamoja na fursa mbalimbali za uchumi ambapo mpakasasa halmashauri zote tano zimepewa eneo la ekari tatu kila moja karibu naKimondo.
Aidha mpango huo umeungwa mkono na wafanyabiasharamkoani Songwe ambao wamesema fursa hiyo itaongeza uchumi wao huku wakiombakuwekewa mazingira wezeshi kwa ajili ya uwekezaji ikiwa ni pamoja na kupewamaeneo ambayo yamekwisha pimwa na kulipwa fidia.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.