SERIKALI YATOA WITO KWA WANANCHI KUTUMIA HIARI YAO KUJITOKEZA KUPATA CHANJO YA UVIKO-19.
SONGWE: Serikali ya Mkoa wa Songwe imetoa wito kwa wananchi wa Songwe kutumia hiari yao kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO-19 kwa ajili ya kupunguza madhara yanayotokana na UVIKO-19.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Momba, Fack Lulandala wakati alipowaongoza wananchi wa Songwe katika zoezi la kupata chanjo ya UVIKO-19 alipomuwakilisha Mkuu wa Mkoa.
"Nimeamua kupata chanjo ya UVIKO-19 si kwamba mimi ni Mkuu wa Wilaya bali kwa sababu nimejiridhisha Usalama na umhimu wa chanjo Iko salama" Fack Lulandala.
Mkuu wa Wilaya amewatoa hofu wananchi kuhusu Usalama wa chanjo na ameeleza kuwa ata wao viongozi wanayapenda maisha na wasingeweza kupata chanjo ambayo ina hatarisha maisha.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ametoa wito kwa watalamu wa Afya, viongozi wa Dini na Mila kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umhimu na faida ya chanjo ya UVIKO-19 na wananchi wajue ukweli wa njia nzuri na Sahihi ya kukabiliana na UVIKO-19 ni njia zinazopendekezwa kitalamu kama vile wanapopatwa na matatizo ya Afya wanapokimbilia kwa watalamu wa Afya.
"Hakuna chanjo ambayo iliwai kufika kwa mara ya kwanza na wananchi wakaipokea vizuri, iwe chanjo au dawa yeyote inapokuwa ndio mara ya kwanza machoni mwa wananchi wanahitaji elimu zaidi ili waweze kuitumia" Fack Lulandala.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Hamad Nyembea amesema Nchi ambazo wameanza kutoa chanjo ya UVIKO-19 vifo na maambukizi yamepungua.
Dkt. Nyembea amesema kwa sasa Mkoa umepokea chanjo ya awali dozi 10,000 ambazo zitagawia kwa kila Halmashauri na wataanza na makundi Maalumu ya wazee, watumishi wa Afya na wenye magonjwa sugu.
Mwenyekiti wa viongozi wa Mila Mkoa wa Songwe, Chifu Mweleshela Nzunda amesema pamoja na wao kuendelea na njia za kijadi za kupambana na UVIKO-19 lakini viongozi wa mila wameipokea vizuri chanjo ya UVIKO-19 baada ya kuona Rais wa Tanzania amepata chanjo na wao watakwenda kufikisha elimu kwa wananchi ili wajitokeze kwa wingi kupata chanjo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Simon Simalenga amesema baada ya kupata chanjo wamejipanga kurudi kwa wananchi na kutoa elimu juu ya faida na umhimu wa chanjo ya UVIKO-19.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Missaile Musa amesema Mkoa umechukua hatua za makusudi za kutoa elimu kwa baadhi ya viongozi wa Dini, Mila na wakisiasa ili waweze kupeleka elimu Sahihi ya chanjo ya UVIKO-19 kwa wananchi na kuwaondolea hofu tofauti na sasa ambapo kuna baadhi ya watu wanapotosha kuhusu chanjo ya UVIKO-19.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.