Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameutaka uongozi wa Mkoa wa Songwe kutumia vyema fursa waliyopata ya kuzindua mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kuutangaza Mkoa wa Songwe.
Waziri Jenista, amesema hayo katika ziara yake ya Siku mbili Mkoani Songwe kuona maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Uhuru Mwenge wa Uhuru utakao fanyika Aprili 2,2019.
Mhe. Jenista amesema Mwenge wa Uhuru unapaswa kuendana na kuzitangaza fursa zilizopo kwenye Mkoa wa Songwe ili taifa na Dunia wajue kwamba Mkoa wa Songwe kuna vitu vizuri.
Pia, Mhe. Jenista amesema Mwenge wa Uhuru ni ishara ya umoja wetu kama Taifa kwani umebeba historia nzuri ya Taifa, uzalendo na jitihada za kujikomboa kiuchumi.
Ameongeza kuwa mwaka huu utakuwa mwaka wa 55 kukimbiza Mwenge wa Uhuru ambao ni ishara ya umoja na alama ya uhuru wa taifa letu.
Wanafunzi zaidi ya mia tisa wakijiandaa na halaiki kwa ajili ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa zitakazofanyika Mkoani Songwe Aprili 2, 2019.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.