Mkoa wa Songwe umekuwa kinara wa kuanzisha utaratibu wa kutoa elimu ya Uzalendo kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari ili kujenga kizazi cha wazalendo wanaoipenda Nchi yao.
Afisa Elimu Mkoa, Juma Kaponda amesema utaratibu huu utakuwa endelevu ijapokuwa sasa elimu hiyo inaanza kutolewa kwa wanafunzi wote wa kidato cha Tano na Sita wa kwa sasa wanaanza na Shule za kidato cha 5 na 6 baadae elimu hiyo itafika kwenye Shule zote za Sekondari.
Kaponda amesema Uzalendo kimsingi ulikua imepotea kwa wanafunzi, Walimu, Wasimamizi wa Elimu, Wazazi na Walezi hivyo elimu ya uzalendo itasaidia kuzua kuendelea kuharibika kwa jamii.
Muelimisha Jamii na Muandishi wa kitabu cha Uzalendo, Joel Arthur Nanauka amewafundisha wanafunzi maana halisi ya uzalendo kwa Nchi, kuijua Nchi yao vizuri, kutokuwa mzigo kwa Nchi, kutoshiriki maovu, kuwasaidia na kutetea wanyonge na wanaoonewa na kujitoa kwa ajili ya Nchi yako.
Nanauka amesema namna ya kuonyesha uzalendo kwa Nchi ni pamoja na kuzungumzia mema ya Nchi, kupenda kuonyesha alama za utaifa kwa kuvaa nguo zenye alama ya Taifa, kutoa ushirikiano kwa viongozi katika shughuli za maendeleo.
Ameongeza kuwa mzalendo anapaswa kununua bidhaa za ndani ya nchi yake, kushiriki kuifanya nchi yake kuwa salama, kushiriki kuchagua viongozi kwa njia ya kupiga kura, kuheshimu sheria za Nchi, kuheshimu na kukubali tofauti baina ya watu, kujitolea kujenga Nchi na kutumia vizuri mali za umma.
Nao wanafunzi waliopata mafunzo ya Uzalendo wameupongeza uongozi wa Mkoa wa Kuona Umuhimu wa wanafunzi kuoata elimu hiyo na kuomba utaratibu huo uwe endelevu na uwafikie wanafunzi wote.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.