• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
SONGWE REGION
SONGWE REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa MKOA WA SONGWE

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Sehemu
      • Mipango na Uratibu
      • Idara ya Elimu
      • Huduma za Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
  • Wilaya
    • Mbozi DC
    • Songwe DC
    • Momba DC
    • Ileje DC
  • Halmashauri
    • Mbozi
    • Ileje
    • Momba
    • Songwe
    • Tunduma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Mifugo
    • Madini
    • Kilimo
    • Biashara
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya na Ustawi Wa Jamii
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma ya Mifugo na Uvuvi
    • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
    • Mipango na Takwimu
    • Ujenzi
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Utaratibu
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TANI 240 ZA MAHINDI ZATAIFISHWA, ZAGAWIWA KWA YATIMA NA SHULE

Posted on: November 13th, 2018

  Tani 240 za mahindi ya chakula zilizokamatwa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kwa kuingizwa nchini kutoka nchi jirani kinyume na taratibu zimetaifishwa na serikali na kugawiwa kwa Vituo vya watoto yatima na shule 18 za sekondari Mkoani Songwe.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela amekabidhiwa mahindi hayo na kufikia uamuzi wa kuyagawa mara baaada ya kujiridhisha kuwa yaliingia nchini kinyume na taratibu na sheria, yametelekezwa kwa muda wa mwaka mmoja na wamiliki wake na bado yanafaa kwa matumizi ya chakula.

“Mahindi haya kisheria nimekabidhiwa baada ya wamiliki wake kushindwa kufuata sheria na taratibu za nchi yetu, yalitoka nchi jirani na yalikuwa yanapelekwa nchi nyingine jirani, TRA wameyataifisha na nimeona tuwagawie wanafunzi wetu na vituo vya watoto yatima wapate chakula kwakuwa mahindi haya tumejiridhisha pia kuwa yanafaa kwa chakula”, ameongeza.

Meneja wa Ushuru wa Forodha wa Kituo cha mpakani cha Tunduma John Masa  amesema bidhaa zote zitakazobainika kusafirishwa kinyume cha taratibu zitataifishwa kama walivyofanya kwenye mahindi hayo baada ya kubaini kuwa yamesafirishwa kwa kukiuka sheria hivyo yamegawiwa kwa Mkoa ambao umetoa kwa wanafunzi na watoto yatima.

Nao baadhi ya wakuu wa shule za sekondari na wawakilishi wa vituo vya watoto yatima ambao wamepokea mahindi hayo ya chakula wameipongeza serikali kwa msaada wa mahindi ambao utasaidia upatikanaji wa chakula katika shule na vituo vyao.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI January 30, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SERIKALI YA SAINI MRADI WA ZAIDI YA BILIONI 119.9 UJENZI WA MRADI WA MAJI TUNDUMA VWAWA

    March 20, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA ILEJE MHE. FARIDA MGOMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA AFUNGUA HUDUMA YA WIKI YA SHERIA MKOANI SONGWE

    January 25, 2025
  • TASAF MKOA WA SONGWE IMEFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI NA KUJIONEA UTOAJI WA HUDUMA KWA WANUFAIKA WA TASAF MOMBA

    January 03, 2025
  • KIKAO CHA TATHMINI YA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO MKOANI SONGWE.

    November 07, 2024
  • Angalia zote

Video

ELIMU KWA WATOTO KIPINDI CHA CORONA
Video za Ziada

Kurasa za Karibu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • SALARY SLIP PORTAL
  • AJIRA

Kurasa Mashuhuri

  • IKULU
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE

    Simu: 025 2580305

    Simu ya Kiganjani: 025 2580305

    Barua pepe: ras@songwe.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.