• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
SONGWE REGION
SONGWE REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa MKOA WA SONGWE

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Sehemu
      • Mipango na Uratibu
      • Idara ya Elimu
      • Huduma za Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
  • Wilaya
    • Mbozi DC
    • Songwe DC
    • Momba DC
    • Ileje DC
  • Halmashauri
    • Mbozi
    • Ileje
    • Momba
    • Songwe
    • Tunduma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Mifugo
    • Madini
    • Kilimo
    • Biashara
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya na Ustawi Wa Jamii
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma ya Mifugo na Uvuvi
    • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
    • Mipango na Takwimu
    • Ujenzi
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Utaratibu
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TANZANIA NI GHALA LA CHAKULA KWA NCHI JIRANI

Posted on: October 23rd, 2018

  Tanzania imeendelea kuwa ghala la chakula kwa nchi jirani kwa kipindi kirefu baada ya kujitosheleza kwa chakula kwa miaka mitano mfululizo na kuweza kuuza ziada ya mazao mbalimbali ya chakula katika nchi za nje.

Kulingana na takwimu zilizotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kipindi cha mwezi Juni 2017 hadi Juni 2018 yameuzwa mahindi kiasi cha Tani 64,477.95  zenye thamani ya Shillingi Billioni 90.6  za kitanzania na maharage  Tani 99,434.45 zenye thamani ya shillingi Bilioni 222.0 za Kitanzania.

Waziri wa Kilimo Dkt Charles Tizeba (Mb), amebainisha hayo wakati akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye kilele cha maadhimisho ya kitaifa ya siku ya Chakula Duniani ambayo yalifanyika kwenye viwanja vya JK Nyerere katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma.

Dkt Tizeba alisema kuwa mazao hayo yamekuwa yakiuzwa zaidi katika nchi za Kenya, Uganda, DRC, Rwanda, Burundi, Sudani Kusini na Uarabuni.

“Pamoja na kuuza mazao nje ya nchi, nchi yetu imekuwa ikitegemea kuagiza zao la ngano kutoka nje ya nchi kutokana na uzalishaji mdogo wa zao hilo hapa nchini. Serikali inatoa wito kwa wakulima hususani wa maeneo ambayo zao hili linalimwa na kukua vizuri waweze kuongeza maeneo ya uzalishaji na tija ili nchi iweze kupunguza utegemezi wa zao hili kutoka nchi za nje” alisema

Ameongeza kuwa pamoja na uzalishaji mzuri wa chakula nchini, Lishe duni (utapiamlo) kwa jamii na kwa baadhi ya maeneo inaendelea kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuathiri maendeleo ya wananchi kiafya, kielimu na kiuchumi.

Aidha, ili kuyafikia malengo endelevu ya maendeleo (Sustainable Development Goals), alisema, Lishe ni moja ya muhimili muhimu wa kuwezesha kufikiwa kwa malengo yote 17 hivyo Serikali kwa kulitambua hilo, imeamua kujumuisha masuala ya lishe kuwa mojawapo ya maeneo ya kimkakati katika Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/17 –2020/21.

Amewataka wadau wote wa lishe nchini kushiriki na kuonyesha bayana mchango wao katika kukabiliana na utapiamlo.

Tarehe 16 ya mwezi Oktoba kila mwaka, Tanzania na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, huadhimisha Siku ya Chakula Duniani ambapo lengo la maadhimisho ya siku hiyo ni kukumbushana wajibu wa kila mmoja katika kupambana na njaa, kuanzia ngazi ya kaya hadi Taifa.

Maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kaulimbiu inayosema, “Matendo yetu ni hatima yetu. Dunia bila njaa ifikapo 2030 inawezekana”. “Kaulimbiu hii inatutaka kufanya kazi kwa umahiri mkubwa ili tujitosheleze kwa chakula na kuwa na akiba ya kutosha kuendesha maisha yetu ya kila siku.” Alisisitiza Dkt Tizeba na kuongeza kuwa,

“Pia kaulimbiu hii inatukumbusha kuacha kufanya mambo kwa mazoea na badala yake tutumie utalaamu katika kuongeza uzaishaji wa mazao  ya kilimo, mifugo na uvuvi.”


Habari na  Mathew Canal

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI January 30, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SERIKALI YA SAINI MRADI WA ZAIDI YA BILIONI 119.9 UJENZI WA MRADI WA MAJI TUNDUMA VWAWA

    March 20, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA ILEJE MHE. FARIDA MGOMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA AFUNGUA HUDUMA YA WIKI YA SHERIA MKOANI SONGWE

    January 25, 2025
  • TASAF MKOA WA SONGWE IMEFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI NA KUJIONEA UTOAJI WA HUDUMA KWA WANUFAIKA WA TASAF MOMBA

    January 03, 2025
  • KIKAO CHA TATHMINI YA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO MKOANI SONGWE.

    November 07, 2024
  • Angalia zote

Video

ELIMU KWA WATOTO KIPINDI CHA CORONA
Video za Ziada

Kurasa za Karibu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • SALARY SLIP PORTAL
  • AJIRA

Kurasa Mashuhuri

  • IKULU
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE

    Simu: 025 2580305

    Simu ya Kiganjani: 025 2580305

    Barua pepe: ras@songwe.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.