TASAF KUONGEZA RUZUKU KWA KAYA ZENYE WALEMAVU.
Na. Nicholas Ndabila
SONGWE: Watalamu kutoka Mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF wanafanya uhakiki wa kaya zinazonufaika na TASAF ambazo zina watu wenyeulemavu kwa lengo la kuwaongezea ruzuku ili kuinua kipato kwa kaya hizo.
Mratibu wa TASAF Mkoa wa Songwe, Bi. Atusungukye Dzombe amesema baada ya Serikali kuona kaya zenye watu wenyeulemavu zina mahitaji makubwa ya kumudumia mlemavu ikaamua kuja na Mpango wa kuongeza Fedha maana ya ruzuku kwa kaya za izo.
"Watalamu wanafanya uhakiki kupita Kwenye kaya za wanufaika au kufanya mikutano ya hadhara ya kijiji kwa lengo la kujjridhisha kama kweli kaya hizo zina watu wenyeulemavu ambao wanaostahili kupata ruzuku" Bi. Atusungukye Dzombe.
Serikali itatoa ruzuku hiyo kwa kaya wanufaika zenye walemavu baada ya kukamilisha zoezi la uhakiki na kaya zitakazokizi kupitia mfumo wa kielotriniki, lengo la kusaidia kaya hizo ili kuboresha Afya, Lishe pamoja na Elimu kwa kaya wanufaika.
"Fedha hizi zimewekewa mfumo mzuri wa usimamizi kuanzia ngazi ya mkoa mpaka ngazi ya chini kabisa ya kijiji kuna timu za uratibu ambazo zinasimamia wakiwemo viongozi wa serikali za vijiji"
Bi. Atusungukye Dzombe.
Serikali inatoa fedha zaidi ya shilingi Bilioni 6 kwa kaya wanufaika 28,474 katika vijiji vyote vilivyopo kwa Mkoa wa Songwe.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.