Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Mkoa wa Songwe, Edwin Kabambagusha, amefanya ziara ya kuwatembelea wanufaika wa mpango wa TASAF pamoja na kukagua miradi inayotekelezwa na wanufaika katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba. Ziara hiyo ilianza tarehe 2 Januari 2025 na kuhitimishwa tarehe 3Januari 2025, ikilenga kufuatilia utekelezaji wa miradi na kuhakikisha kuwa fedha za TASAF zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
9G2A5407.jpg
|
9G2A5360.jpg
|
Kabambagusha alipata fursa ya kuzungumza na wanufaika, kuona maendeleo ya miradi mbalimbali, na kutoa maelekezo ya namna bora ya kuimarisha utekelezaji wa mpango huo. Ziara hiyo inalenga kuongeza ufanisi wa miradi na kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea kunufaika na mpango wa TASAF kwa kuboresha maisha yao.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.