Mkuu wa mkoa wa Songwe,Dk Francis Michael Katikati, Katibu Tawala mkoa wa Songwe Bi. Happiness Seneda (wa kwanza kutoka upande wa Kulia) na Mkurugenzi wa wilaya ya Songwe.
Dk Francis amesema kuwa Mwenge wa Uhuru 2023 utapitia miradi 47 yenye thamani ya Sh15.5 bilioni katika mkoa huo.
Dk Michael amesema hayo baada ya kupokea Mwenge wa Uhuru kimkoa leo Jumamosi asubuhi Septemba 2, 2023 kabla ya kuanza kukimbizwa katika Wilaya ya Momba.
"Tumeupokea Mwenge wa Uhuru ukiwa salama na utakimbizwa Kilometa 722 na utapitia miradi 47 yenye thamani ya Sh15.5 bilioni" amesema Mkuu huyo wa Mkoa.
Dk Michael amesema kuwa baadhi ya miradi itazinguliwa, kuwekewa mawe ya msingi na kutembelewa.Mwenge huo wa Uhuru 2023 umepokelewa leo eneo la Kamsamba Wilayani Momba kabla ya kuanza kukimbizwa katika Halmashauri zote tano za mkoa huo.
Baadhi wa viongozi waliofika ni pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Happiness Seneda, Wakuu wa wilayaza na Wakurugenzi, makatibu tawala wa wilaya za Halmashauri za Mkoa wa Songwe, viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi, wafanyakazi na wananchi.
Baada ya Mwange huo wa Uhuru kukabidhiwa katika Mkoa wa Songwe umeanza kukimbizwa katika Halmashauri tano za Mkoa wa Mkoa wa Songwe ukianza na Momba, Songwe, Mbozi, Tunduma na kuhitimishwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.