THPS YABORESHA HUDUMA ZA KIFUA KIKUU MIKOA YA SONGWE, KATAVI, RUKWA NA KIGOMA.
SONGWE: Tanzania ni miongoni mwa Nchi 30 zinazochangia 87% ya wagonjwa wa kifua kikuu Duniani na inakadiriwa kuwa kati ya watu 100,000 watu 237 wanaugua kifua kikuu kila mwaka Tanzania na kwa mujibu repoti ya shirika la Afya Duniani (WHO) ya 2020 Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa 137,000 waliogua kifua kikuu na 2019 waligundulika wagonjwa 81,208 ikiwa ni ongezeko la 5,363 kutoka 78,845 ya waliogundulika 2018 ambayo ni sawa na 59% na hivyo kuwa na takribani 41% ya watu ambao wanamaambukizi ya kifua kikuu lakini hawajatambulika Tanzania.
Kwa sababu hiyo, Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) limeboresha huduma ya tiba ya kifua kikuu kwa Mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa na Songwe kwa kuwakabidhi vifaa tiba vya vya kuchunguza ugonjwa wa kifua kikuu vya thamani ya Milioni 420 ambavyo vimekabidhiwa Mkoa wa Songwe kwa niaba ya Mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma.
Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Songwe ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Cosmas Nshenye amepokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mikoa hiyo katika hafla iliyofanyika katika Zahanati ya Mlowo Wilaya ya Mbozi leo Agosti 4.
Vifaa vilivyotolewa na THSP ni Mashine za Genaexpert 8 za kutambua Kifua kikuu ambayo moja inauzwa Milioni 44 kila Mkoa utapata mashine 2 gharama ya mashine ni Milioni 355 pamoja na Hadubini (Led microscope)11 kila moja in Milioni 5.9 sawa na Milioni 65 jumal ya vifaa vyote ni thamani ya Milioni 420.
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Missaile Musa amewataka watumishi wa Afya kuvitunza vifaa hivyo kwani vifaa vikitokewa na wadau Kwa Serikali vinakuwa ni mali ya Serikali na vinatakiwa kutunzwa vizuri na kuwahudumia wananchi kwa ufasaha.
George Musyani, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbozi, ni miongoni mwa wananchi ambaye ameuguza ndugu yake kwa muda mrefu bila kugundua kama ana kifua kikuu kwa sababu ya Kukosekana kwa vifaa tiba ambayo vinaweza kugundua kifua kikuu hadi pale alipoenda Mkoa wa Mbeya na kubaini ndugu yake ana kifua kikuu, hivyo amewashukuru wadau kwa kufanikisha vifaa vya Genaexpert kwa Mkoa wa Songwe kwani vitakwenda kusaidia kugundua matatizo ya kiafay kwa wananchi haswa wale wenye kifua kikuu kilichojificha.
"Mwaka 2019 Mkoa wa Songwe ulikuwa na mgonjwa mmoja sugu wa kifua kikuu lakini 2020 walipatikana wagonjwa 6 sugu na hii ni hatarii wanapokuwa kwenye jamii bila kugundulika, hivyo ni matarajio yangu vifaa hivi vitakwenda kufanya kazi ya kuwagundu wagonjwa wa kifua kikuu mapema na kwa Haraka" Cosmas Nshenye Mkuu wa Wilaya ya Mbozi.
Mkoa wa Songwe 2020 ulifanikiwa kugundua wagonjwa 715 wa kifua kikuu sawa 83%, Hii inaonyesha Mkoa bado unawagonjwa wa kifua kikuu lakini bado hawajatambuliwa na kusababisha kuambukiza watu wengine.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.