• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
SONGWE REGION
SONGWE REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa MKOA WA SONGWE

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Sehemu
      • Mipango na Uratibu
      • Idara ya Elimu
      • Huduma za Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
  • Wilaya
    • Mbozi DC
    • Songwe DC
    • Momba DC
    • Ileje DC
  • Halmashauri
    • Mbozi
    • Ileje
    • Momba
    • Songwe
    • Tunduma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Mifugo
    • Madini
    • Kilimo
    • Biashara
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya na Ustawi Wa Jamii
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma ya Mifugo na Uvuvi
    • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
    • Mipango na Takwimu
    • Ujenzi
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Utaratibu
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TRA SONGWE YAGAWA BIDHAA ZILIZOINGIZWA KWA NJIA ZA MAGENDO

Posted on: March 4th, 2020

  Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) Mkoa wa Songwe imegawa baadhi ya bidhaa zilizo kamatwa kwa kuingizwa Nchini kupitia mpaka wa Tunduma kwa njia za Magendo ili kukwepa ushuru.

Akipokea bidhaa hizo kutoka Kwa Kaimu Meneja TRA Mkoa wa Songwe, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela amesema bidhaa hizo zinapelekwa katika shule za Sekondari za Mkoa wa Songwe ili ziweze kuwasaidia wanafunzi.

“Nimepokea simenti mifuko 192, mafuta ya kupikia ndoo 37 na sukari katoni 70 ambavyo vyote navielekeza katika shule za Sekondari  ili vikasaidie huko.” , amesema Brig. Jen. Mwangela.

Amesema mifuko 100 ya simenti ameelekza ipelekwe Wilaya ya Momba ambapo kuna ujenzi wa shule ya sekondari ya Wasichana kwa kidato cha tano na sita na sukari imetolewa kipaumbele Wilaya ya Mbozi ambayo watakuwa wenyeji wa wanafunzi wa Michezo ya Umiseta.

Brig. Jen. Mwangela amewataka Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanafuatilia bidhaa hizo ili zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Momba Juma Said Irando ametoa wito kwa wananchi na wafanyabiashara waliozoea kutumia njia zisizo halali kuingiza bidhaa nchini Kupitia Mpaka wa Tunduma waache maramoja kwani kamati ya Usalama ya Wilaya yake imeimarisha doria ili kumaliza tatizo la wakwepa kodi.

Irando amewata wafanyabiashara kutumia njia halali pia wazingatie sheria na taratibu za forodha ili waweze kufanya bishara halali na kuepuka hasara kwakuwa watakamatwa.

Amesema kuwa wafanyabiashara watambue kuwa wakikamatwa na bidhaa ambazo zimeingizwa Nchini isivyo halali sio tu watataifishwa mali hizo bali sheria zinawataka walipe kodi na faini ili wachangie pato la Nchi.

Irando ameongeza kuwa Wilaya yake imepokea mifuko 100 ya simenti ambayo itasaidia katika ujenzi wa Sekondari ya Wasichana ambayo itakuwa sekondari ya A level kwa wasichaa pekee Mkoa wa Songwe.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Songwe Farensi Mniko amesema walifanikiwa kukamata bidhaa hizo kutokana na kuimarisha kaguzi mbalimbali katika Mpaka wa Tunduma pia kwa kupata taarifa kutoka kwa wananchi mbalimbali.

Mniko ameongeza kuwa bidhaa zilizo kamatwa zikikaa muda mrefu bila mhusika kuzichukua Kamishna wa TRA anayo mamlaka ya kuzigawa kwa taasisi za serikali kama alivyo fanya kwa bidhaa za simenti, sukari na mafuta alizozitoa.

Ameongeza kuwa bidhaa hizo hukaguliwa ubora wake kabla hazijagawiwa kwa taasisi za serikali hivyo zinakuwa salama, huku akiwasisitiza wafanyabiashara waache kupita njia zisizo halali kwakuwa TRA imejipanga kukomesha magendo.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI DATA CLEARK, CLINICIAN NA NURSE October 01, 2021
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • WANAWAKE WAGUSA MAISHA YA WATU WENYE WAHITAJI

    March 08, 2023
  • WITO WATOLEWA WANAWAKE KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI ZILIZOPO.

    March 06, 2023
  • NIMEKUJA KUBORESHA MAZURI YOTE, RC MICHAEL.

    March 03, 2023
  • TUTAFANYA KAZI NA WADAU WOTE KUTIMIZA LENGO LA SERIKALI: RC MICHAEL.

    March 02, 2023
  • Angalia zote

Video

ELIMU KWA WATOTO KIPINDI CHA CORONA
Video za Ziada

Kurasa za Karibu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • SALARY SLIP PORTAL
  • AJIRA

Kurasa Mashuhuri

  • IKULU
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE

    Simu: 025 2580305

    Simu ya Kiganjani: 025 2580305

    Barua pepe: ras.songwe@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.