TUMIENI FURSA YA KAHAWA KUANZISHA KILIMO CHA PAMOJA, RAS SENEDA.
SONGWE: Wadau wa Kahawa kutoka Mkoa wa Mbeya na Songwe wametakiwa kutumia fursa ya zao la Kahawa kuanzisha kilimo cha pamoja cha mashamba makubwa (Block Farmer) ili waweze kuzalisha kwa tija na uhakika wa soko la Kahawa.
Wito huo umetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Bi. Happiness Seneda wakati akifungua mkutano wa wadau wa Kahawa, 2 Septemba 2022 ambao wamekutana kujadili namna ya kuanza kilimo cha pamoja cha mashamba makubwa (Block Farmaer) kwa kuanzia na zao la Kahawa kupitia vyama vya ushirika vilivyopo katika Mkoa wa Songwe na Mbeya.
Katibu Tawala Mkoa, Bi. Happiness Seneda amesema tija ya uzalishaji wa Kahawa iko chini wakati eneo la kulima Kahawa likiwa linaongezeka lakini uzalishaji wa Kahawa unapungua.
“Mfano kwa msimu wa 2019/2020 lengo za uzalishaji ilikuwa ni tani elfu 15 lakini zikapatikana tani elfu 12, msimu wa 2020/2021 lengo ilikuwa tani elfu 13 zikapatikana elfu 11 na 2021/2022 lengo ilikuwa tani elfu 14 zikapatikana elfu 12” Bi. Happiness Seneda Katibu Tawala Mkoa wa Songwe.
Bi. Happiness Seneda amesema tusipojipanga vizuri kwenye Kilimo cha pamoja (Block Farming) tija ya kahawa ba bei nzuri sokoni itakuwa ni changamoto, ili ndio zao la mkakati kwa Mkoa wa Songwe ambalo linafanya vizuri, hivyo kuliendeleza kwa ufanisi kunahitaji kilimo cha kisasa pamoja na kilimo cha pamoja.
Benjamin Mwangala Mrajis msaidizi Mkoa wa Songwe amesema kuvishirikisha vyama vya ushirika ili viweze kushiriki katika agenda yakuwa na mashamba makubwa ya pamoja (Block Farmer) ni mkakati ifikapo 2030 Kilimo kiweze kuchangia 10% katika pato la Taifa.
Isack Mirai Afisa mradi Shirika la Café Africa Tanzania amesema soko la Kahawa linategemea nje, hivyo kitendo cha Serikali kuhamasisha kilimo cha pamoja ni wazi itasaidia kupata Kahawa iliyo bora na soko lake litakuwa la uhakika, kahawa inayozalishwa katika mashamba ya pamoja inakuwa ubora wake unakuwa na uwiano sawa.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.