TUNZENI CHAKULA NA KUKILINDA NA WEZI MASHAMBANI, RC MGUMBA.SONGWE:
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amewataka wananchi kuchukua tahadhari ya njaa kwenye kaya zao kwa kuepuka kuuza Chakula chote au kutumia Chakula hovyo kwenye mambo yasiyokuwa ya lazima.Mkuu wa Mkoa ametoa wito huo wakati akiongea na wananchi kwenye mikutano mbalimbali akiwa kwenye ziara ya ukaguzi wa miradi na kusikiliza kero za wananchi Wilaya ya Mbozi."Mwaka huu sio mzuri upungufu wa chakula ni mkubwa sana ndani ya Nchi yetu na nje ya Nchi bei za vyakula zitazidi kupanda" Mhe. Omary Mgumba.Inawezekana bei ya sasa ikakuvutia ukaona ni kubwa lakini muda si mrefu bei zitazidi kupanda zaidi hivyo mwananchi kama kunaulazima wa kuuza basi uza kidogo kwa ajili ya kutatua matatizo yako na kuiacha familia salama dhidi ya njaa pamoja na Nchi amesema Mhe. Omary Mgumba.Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wananchi kuunda ulinzi shirikishi wa jadi (sungusungu) kupambana na wezi ambao wameibuka na kuiba mazao yakiwa shambani nyakati za usiku ili kulinda chakula kilichopo kisiibiwe na wezi.MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.