UMASIKINI WATAJWA CHANZO CHA UKATILI KWENYE FAMILIA.
SONGWE: Familia zimehimizwa kufanya kazi kwa bidii na kupambana na umasikini uliopo hili kuepuka ukatili wa kiuchumi na Kijinsia ambao umekuwa ukishamiri kwenye familia nyingi.
Wito huo umetolewa na wajumbe wa kongamano la familia wakati wa wakiadhimisha siku ya Familia Duniani ambalo limefanyika Wilaya ya Mbozi, 15 Mei 2022.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Songwe, Ndg. Elynico Mkola amesema ni vizuri jamii na Serikali kusisitiza kwa nguvu zote watu wafanye kazi hili wapate kipato cha kuhudumia familia zao.
Mkola amesema ata jamii kwa sasa imebadilika inaona Mafanikio ni kitu ambacho kina kuja kwa muda mfupi na sio kufanya kazi.
"Mwanaume kama unaweza kuitunza familia yako hakuna mwanamke mwenye kibuli hivyo hivyo kwa mwanamke ukifanya kazi na ukaweza kumudu familia huwezi kupata ukatili wa aina yeyote kutoka kwa mwanaume, kwani hakuna mwanaume anayedharua mwanamke mwenye fedha" Elynico Mkola.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba ametoa wito kwa familia kukaa pamoja na kujadili namna ya kufanya kazi kwa manufaa ya familia zao.
"Tusivutane mashati kwenye familia kila mmoja ndani ya familia afanye kazi hili kila mtu aweze kujimudu na kuogopa kuwa kupe" Mhe. Omary Mgumba.
Aidhaa, Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa jamii na familia kutokuwa chanzo kwa vitendo viovu kwa kusifia na kushabikia mtu mwizi wa mali za umma hili tuweze kuisadia Taifa na familia.
Pia, ametoa wito kwa akinamama haswa wale ambao wanafanya kazi kuacha ukatili wa kiuchumi kwa wanaume zao kwa madai mshahara wa mwanamke ni wake tu lakini mshahara wa mwanaume ni wao wote jambo ambalo ni ukatili wa kiuchumi kwa wanaume wengi ndani ya familia.
Debora Mhekwa kutoka dawati la jinsia, amesema ukatili wa kiuchumi wanawake wamekuwa waathirika wakubwa haswa katika kipindi hiki cha mavuno ambapo mwenye sauti ya matumizi ya fedha ni baba tu lakini wakati kutafuta wamelima pamoja hali inayopelekea familia kupata ukatili wa kiuchumi.
Nao viongozi wa Dini wametoa wito kwa familia kuwekeza malezi yao juu ya hofu ya Mungu hili kuwa na familia bora na Taifa bora kwenye jamii.
Mchungaji Felix Mbogela amesema mzazi ukipata Mtoto wa kike jua sio wako bali unamuandaa kuwa mke wa mtu na ukipata Mtoto wa kiume jua sio wako bali unamuandaa kuwa mume wa mtu hivyo mzazi unapaswa kumulea Mtoto katika njia ya kumjua Mungu na kuwa na hofu ya Mungu.
"Tukiwalea watoto vizuri wenye hofu ya Mungu tutapata viongozi bora wa Taifa, tutapata watumishi bora serikalini hili Taifa la Tanzania liendelee kuwa bora"
Sheikh Yusuph Ally, amesema kila moja kwenye familia ni mchunga katika familia yake uwe mama, baba hivyo mwanaume hupaswi kufanya vitu pekee yako bila kushirikisha familia yako.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.