Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu, Ndg. John Mwaijulu, akiwa mgeni rasmi akimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Songwe, Mhe. Dkt. Francis Michael, amezindua rasmi programu jumuishi ya taifa ya malezi, makuzi, na maendeleo ya mtoto (PJT-MMMAM) kwa mkoa wa Songwe. Programu hii inalenga kutoa huduma jumuishi kwa watoto katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na afya, lishe, fursa za uwekezaji wa awali, malezi ya mwitikio, pamoja na ulinzi na usalama kwa watoto wenye umri wa miaka sifuri hadi nane (0-8).
Uzinduzi huu ulihudhuriwa na wakuu wa dawati la jinsia na watoto, pamoja na wawakilishi kutoka mashirika na taasisi zinazojihusisha na masuala ya watoto. Mashirika hayo ni pamoja na Himso, Children in Crossfire, Tecden, Watoto Wetu,UNICEF, Pamoja na UTCP (Waandishi wa Habari).
Programu hii ni juhudi muhimu za kuimarisha huduma za kijamii kwa watoto katika mkoa wa Songwe na inalenga kuhakikisha kuwa watoto wanapata fursa bora za makuzi na malezi, pamoja na ulinzi dhidi ya hatari zozote zinazoweza kuwakabili. Uzinduzi huu ni hatua muhimu katika kuhakikisha ustawi na maendeleo bora ya watoto katika mkoa katika mkoa wa Songwe.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.