Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela amewataka wafanyabiashara na watumiaji wa soko la Halmashauri ya Mji Tunduma kuzingatia uvaaji wa barakoa ili kujilinda na kuwalinda watu wengine dhidi ya Ugonjwa wa Corona.
Brig. Jen. Mwangela ameyasema hayo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika soko hilo na kukuta wananchi na wafanyabiashara wengine wanazingatia kunawa maji tiririka na sabuni pia wanaa vitakasa mikono lakini hawakuvaa barakoa.
Amesema uvaaji wa barakoa nia agizo la serikali kufuatia ushauri wa watalamu wa afya kuwa njia mojawapo ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona ni kuvaa barakoa.
Aidha, Brig. Jen. Mwangela amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma kuchukua hatua za haraka za kuhakikisha elimu inatolewa kwa wananchi ili wavae barakoa katika maeneo ya sokoni, stendi na katika mikusanyiko mingine.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.