VIJANA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI.
Na. Nicholas Ndabila.
SONGWE: Mkuu wa mkoa wa Songwe Mhe. Waziri Kindamba amewataka vijana mkoani Songwe kuchangamkia fursa za kiuchumi zinazoletwa na Serikali ya awamu ya sita katika mkoa wa Songwe ili kujiimarisha kiuchumi wenyewe, familia zao na Taifa kwa ujumla.
Mheshimiwa Kindamba amesema hayo Septemba, 9 aliposhiriki Swala ya pamoja na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Mskiti wa Masijid Noor uliopo mji wa Vwawa Wilayani Mbozi.
Amezitaja baadhi ya fursa kama vile Kilimo, ufugaji, utalii, uchimbaji wa madini, Biashara, fursa ya Mkoa wa Songwe kupakana na Nchi ya mbili ya Zambia na Malawi na kuufanya Mkoa kuwa lango kuu la Nchi za ukanda wa Afrika kusini.
Mhe. Kindamba amesema kwa sasa mpango wa Serikali ni kuwa na Bandari kavu katika mji wa Tunduma, hivyo ametoa wito kwa vijana kuhakikisha wanakuwa miongoni mwa watu ambao watanufaika na uwepo wa Bandari kavu pamoja na fursa nyingine.
"Namuomba mwanyezi Mungu kwa muda wote nitakapo kuwa hapa anijalie nizitengeneze fursa nyingi kwa vijana wa Songwe na vijana kweli mzichangamkie fursa izo" Mhe. Waziri Kindamba Mkuu wa Mkoa wa Songwe.
Aidha Sheikh wa Mkoa wa Songwe Sheikh. Husein Butuza amesema baadhi ya mikakati wanayo fanya ni pamoja na ujenzi wa kituo cha Afya katika Mji wa Tunduma ili kusaidiana na Serikali katika utoaji wa huduma za Afya.
Mhe. Kindamba amesema ataendelea kushirikiana na Dini zote ili kuhakikisha Mkoa una piga hatua mbele kimaendeleo.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa amewaomba waumini kuendelea kupata chanjo ya UVIKO-19.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.