VIJANA WEKEZENI KWENYE KILIMO, RC KINDAMBA.
Na. Nicholas Ndabila
SONGWE: Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Waziri Kindamba amewataka vijana wajasilimali kuchangamkia fursa ya mikopo inayotolewa kwenye Taasisi za kifedha na kuwekeza katika sekta ya Kilimo.
Mkuu wa Mkoa ametoa wito huo, 5 Oktoba alipotembelea baadhi ya Taasisi za kifedha za CRDB, NMB pamoja na NSSF zilizopo wilayani Mbozi kujionea jinsi zinavyotoa huduma kwa wananchi ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja iliyoanza Oktoba 3 na kuhitimishwa Oktoba 9.
Mhe. Kindamba amewataka vijana kutoogopa kuchukua mikopo ila wachangamkie fursa katika sekta ya Kilimo kwa kuwa Mkoa wa Songwe una fursa kede kede za kuwekeza kwenye Kilimo.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. WaziriKindamba ametoa wito kwa vijana kujihusisha zaidi na shughuli za uzalishaji mali kwa ajili ya kujiletea maendeleo na kujiepusha na mambo hatarishi ya starehe na anasa kwani kufanya hivyo vijana hao hugeuka mzigo kwa familia zao na Taifa kwa ujumla.
Pamoja na mikopo inayotolewa kwenye Taasisi za kifedha, Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluh Hassan kupitia Halmashauri wanatoa mikopo isiyokuwa na riba kwa vijana, wanawake na wenyeulemavu ambayo vijana wanaweza kutumia fursa ya mikopo hiyo kuwekeza katika sekta ya Kilimo.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.