Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela amewaagiza viongozi wa minada kuhakikisha wafanya biashara kwenye minada wanakuwa na vitambulisho vya ujasiliamali ambavyo kwa sasa vinakuwa na picha ya mfanyabiashara husika.
Brig. Jen. ametoa wito huo alipokuwa anaongea na viongozi wa mnada wa Ndalambo uliopo Wilaya ya Momba uliofanyika, 13 Aprili 2021.
Amesema watendaji wa Halmashauri wanapaswa kwenda kwenye minada kuwafuata wafanyabiashara kwa ajili ya kuwaelimisha na kuwapatia vitambulisho vya wajasiriamali wadogo.
Brig. Jen Mwangela ameongeza kuwa ni marufuku viongozi wa minada kuwa wakazi wa nje ya Mkoa kwani wanatakiwa viongozi wote wawe wa wakazi wa Mkoa wa Songwe ili waweze kuendeleza minada kwa ufanisi.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.