• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
SONGWE REGION
SONGWE REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa MKOA WA SONGWE

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Sehemu
      • Mipango na Uratibu
      • Idara ya Elimu
      • Huduma za Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
  • Wilaya
    • Mbozi DC
    • Songwe DC
    • Momba DC
    • Ileje DC
  • Halmashauri
    • Mbozi
    • Ileje
    • Momba
    • Songwe
    • Tunduma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Mifugo
    • Madini
    • Kilimo
    • Biashara
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya na Ustawi Wa Jamii
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma ya Mifugo na Uvuvi
    • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
    • Mipango na Takwimu
    • Ujenzi
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Utaratibu
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAALIMU WATORO NA WACHELEWAJI KUCHUKULIWA HATUA

Posted on: October 22nd, 2019

  Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela amefanya ziara ya kushtukiza katika baadhi ya shule za Msingi na Sekondari na kisha kumuagiza Afisa Elimu Mkoa kuwachukulia hatua za kinidhamu waalimu wote ambao wanachelewa au kutohudhuria shuleni.

Brig. Jen.  Mwangela ametoa agizo hilo mapema leo mara baada ya kutembelea shule za sekondari za Myovizi na Simbega pamoja na Shule ya Msingi Iyula za Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi na kubaini utoro na uchelewaji wa waalimu mara baada ya kukagua madaftari ya mahudhurio.

“Mahudhurio ya waalimu sio mazuri, waalimu hawafiki wote katika shule zao na wengine huchelewa sana, pia vitabu vya mahudhurio havijafungwa ifikapo saa moja na nusu na saa moja na dakika 45 kama inavyotakiwa ili kuwabana wachelewaji.”, amesema Brig. Jen.  Mwangela.

Brig. Jen.  Mwangela amesema Afisa Elimu Mkoa anapaswa kusimamia mahudhurio ya waalimu kwakuwa msingi wa taifa unajengwa shuleni na msingi huo hauta imarika endapo waalimu watakosa nidhamu katika kuwahi na kuhudhuria shuleni.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Myovizi Tabu Mtafya amesema amekuwa akitoa onyo kwa waalimu ambao wanachelewa hivyo agizo la Mkuu wa Mkoa ataendelea kulitekeleza.

“Baada ya Mkuu wetu wa Mkoa kukagua kitabu cha Mahudhurio ameniagiza niendelee kusimamia mahudhurio ya waalimu, nami nitawaita waalimu wote wa shule yangu niwakumbushe juu ya kuwahi na kutimiza wajibu wao.”, amesema Mtafya.

Mkuu wa Wilaya ya Mbozi John Palingo amekiri kuwepo kwa mapungufu ya waalimu kutohudhuria au kuchelewa shuleni na hivyo wamejipanga katika Wilaya ya hiyo kusimamia mahudhurio ya waalimu na kwachukulia hatua za kinidhamu waalimu watoro na wachelewaji.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI January 30, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SERIKALI YA SAINI MRADI WA ZAIDI YA BILIONI 119.9 UJENZI WA MRADI WA MAJI TUNDUMA VWAWA

    March 20, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA ILEJE MHE. FARIDA MGOMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA AFUNGUA HUDUMA YA WIKI YA SHERIA MKOANI SONGWE

    January 25, 2025
  • TASAF MKOA WA SONGWE IMEFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI NA KUJIONEA UTOAJI WA HUDUMA KWA WANUFAIKA WA TASAF MOMBA

    January 03, 2025
  • KIKAO CHA TATHMINI YA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO MKOANI SONGWE.

    November 07, 2024
  • Angalia zote

Video

ELIMU KWA WATOTO KIPINDI CHA CORONA
Video za Ziada

Kurasa za Karibu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • SALARY SLIP PORTAL
  • AJIRA

Kurasa Mashuhuri

  • IKULU
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE

    Simu: 025 2580305

    Simu ya Kiganjani: 025 2580305

    Barua pepe: ras@songwe.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.