WADAU WATAKA KUONGEZWA KWA VITUO VYA KUGAWA MBOLEA ZA RUZUKU.
SONGWE: Wadau wa kilimo Mkoani songwe wamewataka mawakala wa mbolea za ruzuku kuongeza idadi ya vituo ili kuwafikia wananchi wanaoishi maeneo ya vijijini.
Hayo yamesema wakati wa kikao cha kufungua msimu wa kilimo kwa mwaka 2022/23 kilicho fanyika Septemba 22 na kuhudhuriwa na makampuni ya mbolea, kampuni ya mbegu, maafisa kilimo, wakulima na Asasi za Kirai zinazojishughulisha na Kilimo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Cosmas Nshenye ambaye ni muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Songwe amesema kitendo cha Mkulima wa Utambalila kufuata Mbolea ya Ruzuku umbali wa KM 70 atajikuta Mbolea amenunua kwa zaidi ya Bei ya Ruzuku ambayo Serikali imeweka.
Mhe. Cosmas Nshenye amewataka makala waliopewa kazi na Serikali ya kuuza Mbolea za Ruzuku kuongeza vituo zaidi karibu na wananchi ili kuwapunguzia mzigo.
"Mnaweza kuvitumia ata vyama vya ushirika ambayo viko karibu na wakulima kwa ajili ya kuuza Mbolea ya Ruzuku, kikubwa mawakala muangalie usalama wenu wa fedha" Mhe. Cosmas Nshenye.
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Bi. Lydia Shonyela amewashauri mawakala kutumia maghala yaliyopo kwenye kila Kijiji kwa ajili ya kuuza Mbolea za Ruzuku ili kuwasaidia wakulima.
Julius Livingstone Afisa masoko wa kampuni ya ETG amesema Kampuni yao watajitahidi kuongeza na sehemu ambayo wakala watashindwa kufika kampuni itaona namna ya kumsaidia usafiri wakala lengo ni kuhakikisha Mbolea inawafikia wakulima wote kwa wakati.
Afisa Masoko Kampuni ya YARRA, Bi. Mwajuma Mwangu amesema ipo haja kwa makampuni ya mbolea kukaa pamoja kuhakikisha Bei ya Ruzuku kwa wateja wanaopatikana maeneo ya vijijini wapate Mbolea ya Ruzuku kwa bei sawa na mjini na kuepsha mkanganyiko kwa wananchi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe, Ndg. Ellynico Mkola amesema vituo vingi vya mawakala vinapatikana mjini na kuwasahau wananchi wanao ishi maeneo ya vijijini ambako ndiko kuna maeneo makubwa ya kilimo.
Pia, Ndg. Mkola ametoa wito kwa wakulima wenzake kutumia vizuri fursa ya Mbolea ya Ruzuku kwa kuongeza tija kwenye mazao ili kuweza kumuunga mkono kwa vitendo Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluh Hassan kwa kutoa Ruzuku ya Mbolea.
Mwenyekiti wa TCCA Mkoa wa Songwe, Ndg. Charles Chenza ametoa wito kwa wakulima kulima mazao zaidi ya moja ili kuweza kutumia vizuri fursa ya Mbolea ya Ruzuku.
Tunaishukuru sana Serikali ya awamu ya sita kwa kuweka Ruzuku ya Mbolea kwa mazao yote, tofauti na miaka ya nyuma Ruzuku ilikuwa inatolewa kwa zao la Mahindi tu, nawaomba wakulima wenzangu tulime mazao tofauti tofauti kwa kuwa Serikali imesikia Kilimo chetu na Ruzuku ipo kwa mazao yote.
Aidha, Mhe. Cosmas Nshenye amesema Mkoa wa Songwe utakuwa mwenyeji wa maadhimisho ya siku ya Mbolea Duniani itakayofanyika wilayani Mbozi kuanzia tarehe 11 hadi 13 Oktoba yatakayofunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Waziri Kindamba na kufungwa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe.
Serikali ya awamu ya sita imetenga fedha Bilioni 120 kwa ajili ya Mbolea ya Ruzuku ambayo imeanza kutolewa kwa mazo yote.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.