Mkoa wa Songwe umeamua kuhamia digitali kwa kuachana na matumizi ya Makabrasha na badala yake kutumia simu (Tablets). akizungumza wakati akikabidhi vitendea kazi hivyo kwa Waheshimiwa wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Chiku Gallawa alisema "Gharama za kuandaa taarifa za vikao vya Waheshimiwa Madiwani na kusambaza ni kubwa pia huchukua muda mrefu, hivyo kwa kuhamia digitali itapunguza gharama za uendeshaji shughuli hizo na kukomboa wakati" alisisitiza.
Mkuu wa Mkoa alisema zoezi la kukabidhi vitendea kazi hivyo litaenda sambamba na ziara zake ambazo anafaya katika kila Halmashauri za Mkoa wa Songwe. vilevile alisema kazi ya mafunzo ya matumizi ya vitendea kazi hivyo itakuwa endelevu kwa kuwatumia Maafisa TEHAMA katika Halmashauri zao
Aidha Mkuu wa Mkoa alisema juhudi ya kutafuta vitendea kazi vingine inaendelea kwani anataka Mkoa utumie mikutano kwa njia ya digitali ( Teleconference). alisema kuwa njia hiyo itapunguza gharama na muda wa kusafiri kwenda Mkoani badala ya kutoa huduma kwa Wananchi katika maeneo yake.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.