WAISLAMU SONGWE WAMETAKIWA KUISADIA SERIKALI KULINDA NA KUTUNZA AMANI ILIYOPO.
SONGWE: Waumini wa Dini ya Kislamu Mkoa wa Songwe wametakiwa kuisadia Serikali katika kulinda Amani iliyopo Tanzania na Mkoa wa Songwe.
Wito huo umetolewa na Sheikh wa Mkoa wa Songwe, Hussein Batuza wakati wa swala ya Eid Al-Aldha iliyofanyika katika Mji wa Tunduma.
"Waislamu kama jamii ya watanzania tuendelee kuitunza na kuhifadhi Amani iliyopo ili siku tunaondoka Duniani tunaiacha Amani yetu" Sheikh Hussein Batuza.
Mkuu wa Mkoa amesema Serikali ipo na itaendelea kulinda Usalama wa raia na mali zao pamoja na kulinda mipaka yetu, hivyo hatutaruhusu mtu yeyote kupola mali za mwenzake au kusababisha maumivi kwa mwenzake.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba amesema bila Amani hatuwezi kufanya Ibada, Biashara, Kilimo pamoja na shughuli za kiuchumi haziwezi kufanyika.
"Kuna maneno yanatoka kwa baadhi ya viongozi yenye viashiria vya kupoteza Amani na wanadiriki kuomba vurugu zinazotokea kwenye baadhi ya Nchi zitokee hapa Nchini sisi Waislamu tuyapuuze maneno ayo na tuwaombee wenzetu ili Nchi zao ziwe na Amani kama iliyopo Tanzania" Omary Mgumba.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wafanyabiashara na wawekezaji kuwekeza Songwe kwakua Serikali inaendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji kama kuimarisha huduma za Afya, Maji, Ulinzi na kujenga bandari kavu kwa Mji wa Tunduma.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.