WAKUU WA WILAYA WATAKIWA KUJIELEZA KUTOSHIRIKI SHUGHULI YA MKOA YA MAZINGIRASONGWE:
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amewataka wakuu wa Wilaya ya Momba, Ileje na Songwe kujieleza kwake ndani ya saa 24 kwa nini hawajahudhuria maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani ambayo kwa Mkoa wa Songwe yamefanyika leo Juni 6 kijiji cha Masangula Wilaya ya Mbozi.Mkuu wa Mkoa ametoa agizo ilo wakati kikao cha majumuisho baada ya kuhitimisha ziara ya siku 4 Wilaya ya Mbozi kilichofanyika mara ya baada ya kumaliza maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani katika ukumbi wa Halmashauri ya Mbozi."Mkoa unapofanya shughuli ya Kimkoa ni lazima viongozi wa kutoka Halmashauri na Wilaya washiriki bila kukosa haiwezekani Mkoa una shughuli alafu Mkuu wa Wilaya au Mkurugenzi na wewe unamambo yako uko hii haikubaliki" Mhe. Omary Mgumba.Mgumba amesema hategemei kuona jambo hili linajirudia tena katika shughuli zote ambazo ni za Mkoa ni lazima viongozi wa Halmashauri na Wilaya washiriki kabla ya hajachukua hatua kali.Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa amewashukuru Uongozi wa Wilaya na Halmashauri ya Mbozi kwa kufanikisha kuandaa maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.