WANAFUNZI 190 KUTOKA MBEYA WATEMBELEA KIMONDO, RC KINDAMBA AWAPONGEZA.
MBOZI: Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Waziri Kindamba amewapongeza wanafunzi wa Shule ya wasichana Ngalijembe iliyopo Mbeya vijijini kwa kuja kufanya utalii Mkoa wa Songwe katika Kimondo cha Mbozi.
Mhe. Kindamba ametoa pongezi alipokutana na wanafunzi hao, 10 Septemba kijiji cha Ndolezi Kata ya Mlangali kilipo Kimondo cha Mbozi ambapo Mkuu wa Mkoa naye alienda kufanya utalii wa ndani kwenye Kimondo.
Pia, Mhe.Waziri Kindamba amewataka wanafunzi hao kuzingatia masomo kwa kuwasikiliza walimu vizuri ili badae Taifa liweze kupata viongozi na watalamu mbalimbali katika fani tofauti.
"Naomba msidanganyike na FATAKI someni sana, kaa mbali na vishawishi" Mhe. Waziri Kindamba.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Cosmas Nshenye amewapongeza wanafunzi hao kwa kuja kukuza uchumi wa Mbozi kwani kila mwanafunzi lazima ataacha fedha Mbozi atanunua soda, juisi na wakazi wa Ndolezi watapata kipato.
Mwalimu Deus Ndimbo kutoka Shule ya wasichana Ngalijembe ametoa wito kwa Uongozi wa Shule nyingine za Mbeya na Songwe kuwaleta wanafunzi wajifunze kwa vitendo kuhusu utalii.
Tumeamua kuwaleta wanafunzi waje watalii kwa vitendo kwani wao ndio warithi wa badae wa utalii juu ya kujua maliasili za Nchi yao.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.