• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
SONGWE REGION
SONGWE REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa MKOA WA SONGWE

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Sehemu
      • Mipango na Uratibu
      • Idara ya Elimu
      • Huduma za Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
  • Wilaya
    • Mbozi DC
    • Songwe DC
    • Momba DC
    • Ileje DC
  • Halmashauri
    • Mbozi
    • Ileje
    • Momba
    • Songwe
    • Tunduma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Mifugo
    • Madini
    • Kilimo
    • Biashara
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya na Ustawi Wa Jamii
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma ya Mifugo na Uvuvi
    • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
    • Mipango na Takwimu
    • Ujenzi
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Utaratibu
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANANCHI 6, WATUMISHI, WENYEVITI WA VIJIJI KITANZINI UHARIBIFU WA MAZINGIRAMBOZI:

Posted on: June 1st, 2022

WANANCHI 6, WATUMISHI, WENYEVITI WA VIJIJI KITANZINI UHARIBIFU WA MAZINGIRAMBOZI:

 Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amemuagiza Kamanda wa Jeshi la Polisi Songwe, kuwatafuta popote pale walipo watu sita (6) ambao wanatuhumiwa  kwa kuhatarisha amani na uharibifu wa mazingira katika msitu wa Namwanga uliopo Kijiji cha Namwanga Kata ya Hezya Wilaya ya Mbozi.Mkuu wa Mkoa amechukua hatua iyo Juni 1 wakati ziara yake baada ya kujionea uharibifu wa mazingira uliofanyika katika msitu wa Namwanga alipokuta miti imekatwa hovyo na uwepo matanuri ya mkaa pembezoni mwa  msitu huo.Watuhumiwa wanaotafutwa ni Eliud Shizya Mwashilindi, Rashid Charles Mwashilindi, Rasco Wiliad Mwashilindi, Michael Pondamali Msukwa, Rapheel Alnasi Mwambala na Yona Watson Mwambala.Waarifu hao wa Mazingira walitaka kuwateka waandishi wa Habari pamoja na kumkamata na kumteka mtumishi mmoja na kushinikiza wamuachie mwenzao aliyekamatwa ndipo watumishi kwa hofu ya maisha ya mwenzao wakamuachia yule muarifuMkuu wa Mkoa amesema Serikali haiwezi kuwaacha waarifu watambe na mazingira yanaharibika na kuonyesha kama wanaweza kufanya kitu chochote ni lazima tuonyeshe Serikali ipo, inafanya kazi, ina meno na haijashindwa kitu chochote"Nimeisha piga marufuku kuchoma mkaa na kukata miti ovyo lakini kitendo kinachofanyika katika msitu wa Namwanga ni kama vile hakuna zuio la aina yeyote hakuna Serikali" Mhe. Omary Mgumba.Mkuu wa Mkoa amemuagiza Kamanda wa Jeshi la Polisi Songwe kuwafungilia kesi za kutishia kuua, uhujumu uchumi, waaribifu wa mazingira pamoja na kuua baadhi ya mifugo ya mwananchi.Mhe. Omary Mgumba amesema watuhumiwa awa sita ndio mwanzo wa kazi ambayo imeanza ya kukomesha uharibu wa mazingira katika msitu wa Namwanga."kwa vitendo hivi vilivyotokea na hali niliyoiona ile ya Uharibifu wa mazingira lazima Serikali ichukue hatua kwa kuwakamata watu wote vinara, viongozi ili watusaidie SeriakliPia, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amemuagiza Katibu Tawala Mkoa wa Songwe kuwasimamisha kazi watendaji wa vijiji vinavyozunguka msitu wa Namwanga, Mtendaji wa Kata ya Hezya, Afisa Tarafa wa Vwawa, Afisa Misitu wa Halmashauri na Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Mbozi.Katibu Tawala wa Mkoa aunde haraka Kamati maalumu ya kuwachunguza watumishi wote waliosimamishwa ili kujua kwa nini hali hii imetokea amesema Mhe. Omary Mgumba."Kwa hali niliyoikuta ya uharibifu wa mazingira ni mbaya sana na kama Rais angekuja leo hapa mie ningechukulia hatua sasa siwezi kuacha hali hii iendelee" Mhe. Omary Mgumba.Aidha, Mkuu wa Mkoa amemuagiza Kamanda wa Jeshi la Polisi Songwe kuwakamata wenyeviti wa vijiji na vitongoji vinavyozunguka msitu wa Namwanga kwa ajili ya kuisadia Serikali kuwapata watu wote wanaoharibu mazingira msitu wa Namwanga.Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Serikali wa siri na Serikali itatunza Siri iyo.MWISHO

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI January 30, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SERIKALI YA SAINI MRADI WA ZAIDI YA BILIONI 119.9 UJENZI WA MRADI WA MAJI TUNDUMA VWAWA

    March 20, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA ILEJE MHE. FARIDA MGOMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA AFUNGUA HUDUMA YA WIKI YA SHERIA MKOANI SONGWE

    January 25, 2025
  • TASAF MKOA WA SONGWE IMEFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI NA KUJIONEA UTOAJI WA HUDUMA KWA WANUFAIKA WA TASAF MOMBA

    January 03, 2025
  • KIKAO CHA TATHMINI YA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO MKOANI SONGWE.

    November 07, 2024
  • Angalia zote

Video

ELIMU KWA WATOTO KIPINDI CHA CORONA
Video za Ziada

Kurasa za Karibu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • SALARY SLIP PORTAL
  • AJIRA

Kurasa Mashuhuri

  • IKULU
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE

    Simu: 025 2580305

    Simu ya Kiganjani: 025 2580305

    Barua pepe: ras@songwe.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.