WANANCHI KARIBUNI MJIFUNZE MATUMIZI SAHIHI YA MBOLEA, RC KINDAMBA.
SONGWE: Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Waziri Kindamba ameawakaribisha wananchi wote kujitokeza kwa wingi katika kusheherekea Maadhimisho ya Siku ya Mbolea Duniani ambayo kitaifa yanafanyika Songwe kuanzia tarehe 11 hadi 13 Oktoba 2022 katika viwanja vya forest Mlowo wilayani Mbozi.
Mhe. Waziri Kindamba amesema hayo leo Oktoba 10 wakati akiongea na wananchi wa Mkoa wa Songwe kupitia Redio ya Vwawa Fm iliyopo Mji wa Vwawa, Wilayani Mbozi.
Maadhimisho yatafunguliwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Waziri Kindamba na mgeni rasimi anategemewa kuwa Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe pia kutakuwa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Mkoa, pamoja na Makampuni mbalimbali, wataalamu na wadau mbalimbali wa kilimo kwa lengo la kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya Mbolea.
Mhe. Waziri Kindamba ametoa wito kwa wananchi wa Songwe wakiwemo Bodaboda, bajaji, daladala, mama ntilie na mahoteli kuchangamkia fursa mbali mbali za kiuchumi zitakazo tokana na ukubwa wa ugeni katika Maadhimisho haya ya siku tatu mfululizo ili kukuza mzunguko wa fedha na kufanya uchumi wa Mkoa wetu Kukua zaidi.
Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Waziri Kindamba ametoa wito kwa wakulima, wananchi kufika na kujifunza matumizi sahihi ya Mbolea ili kufanya Kilimo chenye tija kitakacho chochea maendeleo kwa Mkoa wetu na Taifa kwa ujumla.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.