WANANCHI WAANDALIWE VIZURI KUPOKEA MRADI, RC KINDAMBA.
MBOZI: Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Waziri Kindamba amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Mbozi na Mkurugenzi kuanza kuwaandaa wananchi wa Kijiji cha Iboya kilichopo Kata ya Ihanda kwa ajili kupokea mradi wa mkubwa wa kituo cha kimataifa cha ukaguzi wa magari yanayofanya safari za nje ya Nchi.
Amesema hayo Oktoba 25, wakati akiongea na wananchi wa Iboya eneo ambalo mradi unatarajiwa kujengwa, Serikali ya awamu ya sita ni ya vitendo na inayokwenda kwa kasi katika kutekeleza miradi.
Mhe. Waziri Kindamba amewatoa hofu wananchi juu utekelezaji wa mradi na ametolea mfano wa Barabara ya TANZAM kutoka Tunduma hadi Mbeya kwa muda mrefu imekuwa ikisemwa itajengwa kwa njia 4 lakini chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan sasa inakwenda kujengwa na hii ndio maana halisi ya Kazi inaendelea.
"Mjiandae na fedha ambazo mtapata za fidia kwa ajili ya kuboresha uchumi wa familia zenu, mjiandae na shughuli za kiuchumi ambazo zitakuwa zinafanyika hapa wakati wa utekelezaji wa mradi na baada ya mradi kukamilika" Mhe. Waziri Kindamba.
Mwananchi unaweza kupata milioni 30 za fidia alafu wewe hujawai shika ata milioni, sasa kama hujajiandaa utakuta unachanganikiwa, viongozi mfike hapa muanze kuwaanda wananchi na kuwapa elimu ya fedha amesema Mhe. Waziri Kindamba.
Pia, Mhe. Waziri Kindamba ameitaka TANROADS baada kukamilisha tathinini wawalipe fedha wananchi ili waendelee na maisha mengine.
Kaimu Meneja wa TANROADS Songwe, Mhandisi, Suleiman Bishanga amesema kituo kitakuwa na ukubwa wa umbali wa KM 2 kwa pande zote za Barabara na itachukua mita 300 kila upande wa Barabara.
"Miundombinu itakayojengwa ni Hoteli, maegesho ya magari, mizani ni eneo ambalo litakuwa kiuchumi na wasafirishaji na wasafiri watapumzika" Mhandisi Bishanga.
Meneja wa TANROADS amesema uthaminishaji uanaanza upya, na wiki ijayo kamati za uthaminishaji za kijiji zitaundwa.
Mkazi wa Iboya, Bi. Sister Mwakyusa ameiomba Serikali kufanya haraka kwa tathimini na kuwalipa, wasicheleweshe kama awali walikaa zaidi ya miaka 3 bila kujua kinachoendelea ila kwa kuwa leo mumekuja viongozi wakubwa basi tunaomba mtusaidie jambo likamilike haraka.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.