WANAWAKE WAGUSA MAISHA YA WATU WENYE WAHITAJI
SONGWE: Katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani Machi 8, Wanawake wa Songwe kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wameadhimisha kwa kugusa maisha ya makundi maalumu kwa kuwapatia baiskeli na viti kwa walemavu wenye mahitaji.
Walemavu wamepatiwa vifaa hivyo na Mama Tunu Pinda mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda katika kilele cha siku ya Wanawake Duniani ambayo kwa Mkoa wa Songwe yamefanyika Wilaya ya Mbozi viwanja vya CCM.
Mama Tunu Pinda amewashukuru wanawake wa Songwe kwa hatua hiyo ambayo imegusa maisha ya watu wenye mahitaji kama walemavu.
Hatua nyingine, Mama Tunu Pinda amekabidhi bima za Afya kwa familia zenye mahitaji, kugawa tauro za kike kwa baadhi ya wanafunzi pamoja na kugawa vyeti vya pongezi kwa Wanawake ambao wamekuwa chachu ya maendeleo kwenye kilimo, biashara na jamii.
Pia, Mama Tunu Pinda ametoa wito kwa wanawake kupaza sauti ili kupinga vitendo vya ukatili vinavyofanyika katika jamii dhidi ya watoto na wanawake.
Aidha, amewataka wanawake kutumia fursa ya mikopo inayotolewa na Serikali kupitia 10% za mapato ya ndani ili kuwawezesha kiuchumi.
"Kina mama kopeni msiogope maadamu mnarudisha, kutumia fursa zinazopatikana katika maeneo yetu ili kuanzisha viwanda" Mama Tunu Pinda.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Esther Mahawe ambaye amemuwakulisha Mkuu wa Mkoa wa Songwe ametoa wito kwa wanawake wote kuwaheshimu wanaume kwenye Ndoa bila kujali hali ya maisha aliyonayo mwaume.
Tunajua katika Ndoa Mungu anaweza kupitisha liziki kwa mwanamke, hivyo kwa nafasi iyo tusijisaau na kuanza kumzarau mwaume kisa tu Mungu kapitishia riziki kwako, Mwanaume atabaki kuwa Mwanaume na kichwa cha familia kwenye Nyumba, amesisitiza Mhe. Esther Mahawe.
Wakati mwingine ukitaka kumpa fedha mwaume, tafadhali usimpe mbele ya watoto mpe mkiwa chumbani, kama kuna ujenzi unaendelea mtume akasimamie hii ndio Heshima ambayo tunapaswa kuwapa wanaume wetu ndani ya Familia bila kujali hali yake ya uchumi amesema Mhe. Esther Mahawe.
Mhe. Esther Mahawe amesema heshima yote anayopaswa kupewa Mwanaume ndani ya Familia isije kuwa ya kutoa mwanya wa ukatili kwa mwanamke.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.