KIKUNDI CHA SANAA MPEMBA CHAPATIWA PIKIPIKI (GUTA) KWA AJILI YA MRADI WA USAFI WA MAZINGIRA MPEMBA NA KATETE
Kikundi cha Sanaa cha Top in Songwe Art Group cha Mpemba, Halmashauri ya Mji ya Mji wa Tunduma kimepatiwa Guta na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Chiku Gallawa kwa ajili ya mradi wa kuzoa takataka katika Mitaa za Mpemba na Katete.
Aidha katika Kata hizo mbili kutakuwa na makundi mawili. Kundi la kwanza la wafanya biashara 250 ambao watakuwa wanachangia Shilingi 6,000 kwa mwezi na kundi la pili ambalo ni la Wakazi wa kawaida wapatao 2,000 hawa watachangia Shilingi 1000 kwa mwezi.
Kaimu Mkurugenzi Regina Shashi alisema kuwa biashara kama itakwenda kama ilivyokusudiwa kikundi kitakuwa na uwezo wa kununua Guta moja kila baada ya miezi mitatu na kwa mwaka mmoja wanaweza kuwa na Guta nne.
Akizungumzia upande wa manufaa kwa Wanakikundi, Shashi alisema Wanakikundi watapata posho ya shilingi 40,000 kwa mwezi na kwamba kutakuwa na uhakika wa kugharamia matengenezo ya Guta hilo.
Kaimu Mkurugenzi aliongeza kuwa Halmashauri ya mji wa Tunduma itakuwa karibu na Kikundi hicho ili kutoa elimu zaidi ya ujasiliamali kwamba wanafanya kazi zingine zaidi ya kuzoa Taka, usimamizi wa fedha, matengenezo na shughuli za utawala kwa ujumla.
Pamoja na hayo Shashi alisema kikundi hicho kitakuwa katika nafasi ya kupewa asilimia 10 inayotolewa kwa ajili ya Wanawake na Vijana kwa sababu tayari wana shughuli ambayo inaonekana na kupimika.
Kiongozi wa Kikundi hicho Bariki Mbogela alisema kuwa Guta litakuwa mkombozi wao kwa sababu fedha watazopata zitawasaidia kurekodi kazi zao za sanaa kwenye studio zenye ubora wa juu na kuwapatia wasanii mahitaji ya kila siku.
Afisa Afya wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma Godfrey Simbeye aliongeza kuwa Mradi huo utapunguza gharama za Serikali kuzoa taka kwani eneo la Halmashuri ni kubwa ukilinganisha na uwezo wa Halmashauri, pia alisema kutokana na hali hiyo hali ya mazingira ilikuwa inaharibika kutokana na takataka kuanza kuoza kabla ya kuzolewa hivyo kupelekea hali hatarishi kwa afya ya Watu na viumbe vingine.
Pia aliongeza kuwa Halmashauri imeanza kutoa elimu kwa wamiliki wa Mabasi ya Abiria kuhakikisha wanakuwa na vyombo vya kutupia takakata na hatua kali zitachukuliwa kwa watakaokaidi agizo hilo. Vilevile alisema kuwa Halmashauri imeanza kutengeneza vifaa vya kutupia takataka ili kuweka maeneo ambayo watu wanapita na kuweka matangazo ya namna ya kuweka takataka kwenye vyombo hivyo na kuwa mtu akionekana akitupa atachukuliwa hatua za kisheria.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.