• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
SONGWE REGION
SONGWE REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa MKOA WA SONGWE

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Sehemu
      • Mipango na Uratibu
      • Idara ya Elimu
      • Huduma za Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
  • Wilaya
    • Mbozi DC
    • Songwe DC
    • Momba DC
    • Ileje DC
  • Halmashauri
    • Mbozi
    • Ileje
    • Momba
    • Songwe
    • Tunduma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Mifugo
    • Madini
    • Kilimo
    • Biashara
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya na Ustawi Wa Jamii
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma ya Mifugo na Uvuvi
    • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
    • Mipango na Takwimu
    • Ujenzi
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Utaratibu
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAZIRI MHAGAMA AHIMIZA VIJANA KUWA WAZALENDO KWA NCHI YAO

Posted on: March 30th, 2019

  Na; OWM – KVAU, Kilimanjaro

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amewahimiza vijana kuwa wazalendo na kuithamini nchi yao.

Waziri Mhagama amezungumza hayo wakati wa hafla ya kuwaaga vijana waliopanda Mlima Kilimanjaro tarehe 26 Machi, 2019 Mkoani Kilimanjaro ikiwa ni kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Amesema kuwa, Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere alikuwa kiongozi mzalendo kwa nchi yake na alijali utu na usawa, hivyo ni vyema vijana na vizazi vijavyo wakarithishwa falsafa za Baba wa Taifa.

“Vijana mna kila sababu kuyaenzi matendo ya Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere na Mhasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, Abeid Amani Karume kwa vitendo kwa kuwa ninyi ndio nguzo ya Taifa na mnaelewa vema tulipotoka, tulipo na tunapoenda,” alisema Mhagama

Aliongeza kuwa, Viongozi hawa hawakuwa wabinafsi kwa kujilimbikizia mali na hawakubagua mtu kwa rangi wala kabila bali walijenga Taifa na kudumisha amani na moja.

Aliendele kwa kuwapongeza vijana kwa azma yao ya kuenzi historia na mazuri yaliyofanywa na viongozi hao kwa kupanda mlima Kilimanjaro na kuwatakia baraka waende na kurudi salama.

“Kitendo hiki ni cha kishujaa na uzalendo wa hali ya juu kwa Taifa ikiwa ishara ya kumuenzi Baba wa Taifa,” alieleza Mhagama

Aidha Waziri Mhagama alitoa rai kwa vijana kuwa wazalendo na kuwasihi wafanye kazi kwa bidii ili kujenga Taifa kupitia uchumi wa viwanda utakao ifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Alifafanua kuwa uzalendo lazima ujengwe sambamba na ujenzi wa uchumi wa Taifa, ulinzi na usalama wa Taifa na utunzaji wa tunu za Taifa.

Pamoja na hayo, aliwapongeza na kuwashukuru Viongozi wa Mkoa wa Songwe na Lindi pamoja na uongozi wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) kwa ushirikiano mkubwa na Ofisi yake katika kuwashirikisha vijana kwenye suala hilo.

Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba alisema kuwa tukio hili ni muhimu kwa vijana kutambua historia na mchango wa Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere katika Taifa.

“Tumieni fursa hii kupitia vitabu mbalimbali vya kihistoria ili mjifunze mipango, mwenendo na malengo ya Baba wa Taifa itawasaidia na kuwajengea nafasi nzuri ya kujitambua na kuelewa historia ya Taifa,” alisema Warioba.

Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana, Bw. James Kajugusi alieleza kuwa Baba wa Taifa alianza harakati za kulikomboa Taifa akiwa kijana na aliendelea kufanya hivyo kwa kuwa hamasisha vijana kujenga Taifa lao baada ya kupata uhuru.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI January 30, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SERIKALI YA SAINI MRADI WA ZAIDI YA BILIONI 119.9 UJENZI WA MRADI WA MAJI TUNDUMA VWAWA

    March 20, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA ILEJE MHE. FARIDA MGOMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA AFUNGUA HUDUMA YA WIKI YA SHERIA MKOANI SONGWE

    January 25, 2025
  • TASAF MKOA WA SONGWE IMEFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI NA KUJIONEA UTOAJI WA HUDUMA KWA WANUFAIKA WA TASAF MOMBA

    January 03, 2025
  • KIKAO CHA TATHMINI YA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO MKOANI SONGWE.

    November 07, 2024
  • Angalia zote

Video

ELIMU KWA WATOTO KIPINDI CHA CORONA
Video za Ziada

Kurasa za Karibu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • SALARY SLIP PORTAL
  • AJIRA

Kurasa Mashuhuri

  • IKULU
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE

    Simu: 025 2580305

    Simu ya Kiganjani: 025 2580305

    Barua pepe: ras@songwe.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.