• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
SONGWE REGION
SONGWE REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa MKOA WA SONGWE

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Sehemu
      • Mipango na Uratibu
      • Idara ya Elimu
      • Huduma za Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
  • Wilaya
    • Mbozi DC
    • Songwe DC
    • Momba DC
    • Ileje DC
  • Halmashauri
    • Mbozi
    • Ileje
    • Momba
    • Songwe
    • Tunduma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Mifugo
    • Madini
    • Kilimo
    • Biashara
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya na Ustawi Wa Jamii
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma ya Mifugo na Uvuvi
    • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
    • Mipango na Takwimu
    • Ujenzi
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Utaratibu
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA KUJADILI RIPOTI YA MTHIBITI NA MKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI (CAG) KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA TUNDUMA, AGOSTI 10, 2018

Posted on: August 11th, 2018

  Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali Nicodemas E. Mwangela;

Ninawapongeza kwa kuvuka lengo la makusanyo na kufikia asilimia 104 hii inaonyesha kuwa katika halmashaurii hii Kuna watu waaminifu, wanaofanya kazi kwa bidiii na waadilifu.

Licha ya pongezi ninazowapa na katika mambo mazuri mnayoyafanya bado kuna dosari kadhaa ndio maana kuna hoja 17 za ripoti ya CAG.

Ofisi yangu iko wazi endapo mtendaji yoyote akiwa na lolote ambalo anajua natakiwa nilifahamu ofisi yangu iko wazi masaa 24 siku 7.

Ninaomba ushirikiano wenu na mimi ninaamini katika ushirikiano kwakuwa mtu mmoja hawezi kufanya mambo yote.

Ili tufanye kazi vizuri malengo tuliyojiwekea tuyatekeleze kwa muda uliopangwa, suala la muda ni muhimu sana, watendaji tuweke utaratibu wa kujipangia kila siku utafanya nini na upange muda wa utekelezaji, hii itatusaidia kuenda kwa kasi.

Kuna tatizo kubwa viongozi tunaletewa taarifa na takwimu za uongo ambapo tukifika maeneo husika kujiridhisha tunakuta hali ni tofauti, sasa ninataka tukiomba taarifa mtuletee takwimu za uhakika ili muweze kuepuka baadhi ya hoja.

Kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wataalamu mkisikia kuna ukaguzi wa ofisi ya CAG mnakwepa kwa visingizio vya ugonjwa, likizo na ruhusa.

Naagiza wakurugenzi msitoe ruhusa kwa wataalamu kipindi cha ukaguzi wa CAG mpaka kuwe na sababu za msingi ili wataalamu kutoka ofisi ya CAG wakija wawakute wataalamu husika ambao wanaweza kujibu hoja vizuri.

Ninaelekeza kuwa hoja iliyojibiwa mwaka jana wa fedha isionekane tena kwa mwaka huu wa fedha.

Mkaguzi wa Hesabu kutoka Ofisi ya CAG Joyce Luena;

Halmashauri ya Tunduma ina kesi zenye thamani ya bilioni 1.38 sawa na asilimia 35 ya bajeti ya mapato ya ndani, halmashauri izisimamie kesi hizo kwa umakini ili kuokoa fedha za serikali pamoja na kusimamia mikataba ili kutojiingiza tena katika kesi.

Halmashauri zizingatie maoni ya Mkaguzi wa ndani kwakuwa ndiye anayewapa picha halisi ya utendaji wa halmashauri unaendaje na hivyo kuweza kuzuia baadhi ya hoja.

Watendaji wajikite zaidi kwenye kuzuia hoja na sio kujibu hoja yaani wasiwe mabingwa ya kujibu hoja bali kuzuia hoja.

Halmashauri iendelee kusimamia mipango ya makusanyo ya mapato waliyojiwekea ili waweze kukusanya Zaidi wasitegee kwakuwa walivuka lengo.

Imetolewa Na:

Grace Gwamagobe

Afisa Habari

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI January 30, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SERIKALI YA SAINI MRADI WA ZAIDI YA BILIONI 119.9 UJENZI WA MRADI WA MAJI TUNDUMA VWAWA

    March 20, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA ILEJE MHE. FARIDA MGOMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA AFUNGUA HUDUMA YA WIKI YA SHERIA MKOANI SONGWE

    January 25, 2025
  • TASAF MKOA WA SONGWE IMEFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI NA KUJIONEA UTOAJI WA HUDUMA KWA WANUFAIKA WA TASAF MOMBA

    January 03, 2025
  • KIKAO CHA TATHMINI YA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO MKOANI SONGWE.

    November 07, 2024
  • Angalia zote

Video

ELIMU KWA WATOTO KIPINDI CHA CORONA
Video za Ziada

Kurasa za Karibu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • SALARY SLIP PORTAL
  • AJIRA

Kurasa Mashuhuri

  • IKULU
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE

    Simu: 025 2580305

    Simu ya Kiganjani: 025 2580305

    Barua pepe: ras@songwe.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.